Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari Serikali yasema, ugumu wa maisha unasababisha maradhi ya akili
Habari

Serikali yasema, ugumu wa maisha unasababisha maradhi ya akili

Dk. Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya wa Tanzania
Spread the love

 

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima amesema, magonjwa mengi ya akili, yanatokana na ugumu wa maisha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Dk. Gwajima ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma, leo Jumatano, tarehe 3 Februari 2021, wakati akijibu swali la  msingi la mbunge Viti Maalum, mkoani Dar es Salaam, Mariam Kisangi.

Amesema, baadhi ya watu katika jamii, hawana uwezo wa kuhimili changamoto zinazowakabili hasa za ugumu wa maisha, jambo ambalo limesababisha kupata maradhi ya ugonjwa wa afya ya akili.

Amesema, “kuna watu wanashindwa kukabiliana na changamoto zao, ikiwamo ugumu wa maisha. Hili nalo ni suala la kukaa na jamii, ili ianze kuzichukulia positive (chanya) changamoto hizo na sio kujiwekea msongo wa mawazo hadi kufika huko kusikotakiwa.”

Pamoja na kuhoji chanzo cha ugonjwa wa afya ya akili, Kisangi alihoji mkakati wa serikali wa kuwasaidia watu wenye maradhi hayo.

Akijibu maswali hayo na mengine, Dk. Gwajima ametaja sababu nyingine zinazochangia mtu kupata maradhi ya akili, kuwa ni pamoja na matumizi ya vilevi kupita kiasi ikiwemo bangi na pombe.

Dk. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya

“Naweza nikatoa mifano hai hapa, kuhusu matumizi ya vilevi kupita kiasi, labda bangi na pombe. Kama mwili wako katika mumbile yake unavyo hivyo vinasaba (ugonjwa wa akili), unaweza ukajikuta unaangukia kwenye ugonjwa wa kukosa akili,” ameeleza.

Vilevile, Dk. Gwajima ametaja vitendo vya ukatili, wanavyofanyiwa baadhi ya watu kuwa navyo vinachangia kuwapo kwa tatizo hilo.

Kufuatia changamoto hiyo, Dk. Gwajima amewaomba wabunge kuwa mabalozi wa kukemea vitendo vya ukatili katika maeneo yao.

“Lakini tuna watu wanaishi wanafanyia wenzao vitendo vya ukatili. Naomba sisi wabunge tuwe mabalozi wa kukemea ukatili huu. Sababu tunaweza kusababisha lekea watu wetu kupata msongo wa mawazo na kugeuka kuwa hatari kwa taifa,” amesisitiza.

Aidha, Dk. Gwajima amesema, ugonjwa wa afya ya akili unasababishwa na masuala ya kibaiolojia na mazingira ya mtu anayoishi.

Amesema, “zimetajwa pia sababu za kibaolojia ambazo ni vinasaba ambavyo mtu anaumbwa navyo, unaweza kuwa navyo, lakini usifikie hatua ya kupata huo ugonjwa kutokana na jinsi gani mazingira unayoishi nayo katika jamii yako.  Na wewe mwenyewe yanavyokuandaa kupata au kutopata.”

Akijibu swali na nyongeza la mbunge wa Viti Maalum, Lucy Mayenga, aliyetaka kufahamu serikali imeweka utaratibu wa gani wa kuwasaidia watu wenye ugonjwa huo walioko gerezani, Dk. Gwajima amesema, wizara yake inajipanga kuhakikisha kesi zao zinamalizika haraka.

Lucy Mayenga, Mbunge viti Maalum (CCM)

“Kuhusu suala la pili naomba nilipokee, kweli umuhimu huo upo; tutajipanga kama wizara kuona jinsi gani tunatoa huduma hiyo ya kuharakisha mashauri hayo yanaisha,” ameeleza.

Mayenga alisema kuna changamoto ya watu wenye ugonjwa huo kusota mahabusu kutokana na mashauri yao kuchelewa kutolewa maamuzi.

Awali, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel amesema, serikali itahakikisha kwamba huduma za wagonjwa wa afya ya akili ikiwemo dawa na matibabu, zinatolewa kwa wakati katika ngazi zote.

Naibu waziri huyo amesema, “serikali inahakikisha kuwa huduma hizi zinatolewa katika ngazi zote za huduma afya kuanzia kwenye jamii, ngazi ya afya ya msingi,  mkoa, kanda mpaka hospitali maalumu ya taifa ya afya ya akili.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!