January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yasaini mkataba wa Sh. 89.4 Bil

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania yasaini mkataba wa Sh. 89.4 bilioni kutoka katika Serikali ya Switzerland kwa lengo la kusaidia kukuza na kuimarisha mfuko wa huduma za afya. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Ni mkataba wa miaka miwili ambapo wa kwanza utahusisha Sh. 31.3 bilioni zitakazopelekwa katika mfuko wa pamoja wa afya ambapo mkataba wa pili utakuwa wa Sh. 42.7 bilioni kuhimarisha mifumo ya huduma ya afya.

Akizungumza na wanahabari, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servancious Likwelile amesema kuwa, fedha hizo zitafikishwa sehemu husika ili kukuza sekta ya afya nchini.

Dk. Likwelile amesema kuwa fedha zitakazotokana na mkataba wa pili ambao unalenga kuimarisha mfumo wa huduma za afya, zitapelekwa hasa katika mikoa mitatu ambayo ni Morogoro, Dodoma na Shinyanga kwa lengo la kukuza upatikanaji wa huduma bora za afya.

“Napenda kushukuru Serikali ya Switzerland kwa kutupatia fursa hii ya kusaini makubaliano ya msaada huu hivyo napenda kuthibitishia kuwa, Serikali ya Tanzania itakuwa bega kwa bega kuhakikisha fedha hizi zinaongeza kasi ya huduma bora katika sekta ya afya,” amesema Dk. Likwelile.

error: Content is protected !!