
Dk. Medard Kalemani, Waziri wa Nishati
Spread the love
WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, amesema kuanzia Julai mwaka huu, serikali itasitisha uagizaji wa mita za luku ya umeme kutoka nje ya nchi ili kutoa fursa kwa wawekezaji wa ndani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Dk. Kalemani amesema nia ya serikali ni kutoa nafasi kwa wawekezaji nchini kuanza kuzalisha vifaa hivyo ili kuendana na kasi ya Tanzania wa viwanda.
Waziri huyo amesema kuwa usitishwaji wa kuagiza mita za luku unaenda sambamba na ule wa nguzo za umeme kutoka Afrika Kusini na transfoma kutoka nchini India.
More Stories
Bawacha yasitisha kongamano la siku ya wanawake duniani
Rais Mwinyi amwapisha mrithi wa Maalim Seif
Mrithi wa Maalim Seif aahidi haya