Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yapewa neno ununuzi treni zilizotumika
Habari za SiasaTangulizi

Serikali yapewa neno ununuzi treni zilizotumika

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imeshauriwa kufikiria upya mpango wake wa kununua vifaa vya treni ya umeme vilivyotumika, maarufu kama mitumba, ili kujua kama hauna athari kwa taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ushauri huo ulitolewa jana Jumatatu, tarehe 4 Julai 2022, muda mfupi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kusema Serikali imetoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa hivyo.

Ikiwemo seti za treni 10, vichwa vya treni vipya 17, pamoja na mabehewa ya abiria 57, ambapo baadhi yake vitakuwa vilivyotumika lakini vyenye hali nzuri.

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Humphrey Moshi, ameishauri Serikali iangalie upya uamuzi huo kwani una athari ikiwemo kufungua milango ya rushwa na udanganyifu.

Rais Samia Suluhu Hassan

“Ninavyofahamu kama Serikali hairuhusu kununua magari chakavu, sioni kwa nini wanunue hizo treni chakavu. Hizo chakavu unaweza danganywa kilomita zilizotembea kumbe sio. Ule udanganyifu, mambo ya rushwa zitaingia. Waangalie upya shughuli za manunuzi. Sheria za vyombo vya moto hairuhusu kununua vyombo chakavu. Wasinunue na wakinunua itakuwa suala la rushwa,” amesema Prof. Moshi na kuongeza:

“Mtu anaweza kudanganya bei fulani kumbe siyo. Tunanunua tunaambiwa yametembea kilomita 50,000 kumbe imetembea kilomita 200,000. Hatuna sababu ya kukwepa kununua kipya sababu itatupa vitu vizuri na matengenezo yake yatakuwa madogo kuliko ukichukua ya zamani na hii itaongeza gharama za matumizi ya Serikali. Wahakikishe wanazingatia sheria moja kwa moja bila kukiuka.”

Naye Msemaji wa Sekta ya Miundombinu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Mohamed Mtambo, ameishauri Serikali isitishe mpango huo, badala yake ifanye uchambuzi wa kina kujua athari zake.

“Mchakato huu lazima uangaliwe upya na kwa umakini sana kwa sababu unavyonunua hivi vitu unatuma vigezo kwa mtengenezaji, unamwambia naomba unipe jembe nakwenda kulima kwenye mawe na mtengenezaji atakupa vochwa vya treni kulingana na vigezo vyako ulivyomtumia kulingana na mazingira na hali ya hewa yako,” amesema Mtambo na kuongeza:

“Hivi used vimetengenezwa kwa vigezo vya aliyenunua awali, unaweza kuta yeye ana baridi sana, sisi tunachoshughulika nacho chuma ambacho kinatanuka na kinaathirika na joto. Hili zoezi ni hatarishi na si jambo la kuliendea harakahara bila kulifanyia uchambuzi wa kina.”

1 Comment

  • Duh!
    Kama reli ni mpya, kwa nini mabehewa ni chakavu? Hayo mabehewa yataharibu reli na yatahitaji matengenezo ya mara kwa mara.
    Ni sawa na kujenga barabara mpya na kupitisha magari mabovu…yanadondosha mafuta barabarani, yanazima na kusukumwa pembeni ambako yanaharibu kingo za barabarani.
    Ni heri tujitutumue na kupata mapya na tutoze nauli zote (abiria, mizigo na makanikia).
    Je shirika la reli linapata kiasi gani kwenye usafirishaji wa makanikia?
    Tuache usiri….uwazi mbele daima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!