Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yapangua hoja ya mbunge Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Serikali yapangua hoja ya mbunge Chadema

Upendo Peneza, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema)
Spread the love

SERIKALI imesema, Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM), ni moja ya waajiri walioandikishwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Na kwamba, watumishi wanaofanya kazi katika mgodi huo, wamegawi makundi mawili; walioajariwa moja kwa moja GGM na walioajiriwa na wakandarasi wanaotoa huduma ndani ya mgodi huo.

Kauli hiyo ya serikali imetokana na swali la Upendo Peneza, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) aliyetaka kujua kwamba, serikali inachukua hatua gani kukomesha malalamiko  ya baadhi ya wafanyakazi katika kampuni zilizopo ndani ya mgodi huo.

“Kampuni ambazo zinafanyakazi ndani ya Mgodi wa Geita Gold Mine (Contractors), zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi wanaofanya kazi kwa kutopeleka fedha kwenye Mifuko ya Jamii na kutowapa mikataba, Je, serikali inachukua hatua gani kukomesha malalamiko hayo?” amehoji Peneza.

Serikali ikijibuswali hilo, imeeleza Februari 2020, jumla ya Sh. 5.01 bilioni zililipwa na GGM kama mchango wa Januari 2020 kwa watumishi 2,038.

“Katika mwezi huo huo, jumla ya wanachama 6,128 ambao wameajiriwa na wakandarasi 39, wanaotoa huduma ndani ya mgodi huo, walikuwa wameandikishwa na NSSF na kuchangiwa wastani wa shilingi bilioni 1.3.

“Serikali kupitia OWM-KVAU imekuwa ikifanya kaguzi katika maeneo mbalimbali ya kazi, ikiwemo ya migodini kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wa Sheria za Kazi,” amesema na kuongeza.

“Kupitia Ofisi ya Kazi ya Mkoa wa Geita, ukaguzi katika Mgodi wa “Geita Gold Mine” ikiwemo kandarasi zinazofanya kazi chini ya Kampuni hiyo umekuwa ukifanyika ili kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi katika maeneo hayo.

“Katika kipindi cha mwaka 2019/2020, ukaguzi umefanyika katika Kampuni za Geita Gold Mine, Africa Underground Mining Services, Capital Drilling, GHP Transportaton, Security Group Africa, Fabec Construction, GIPCO Construction, East Africa Radiators, Paulando Enterprises, AVLOW (T) Ltd na EPSON Ltd,” Alisema Wizara.

Aidha,serikali ilisema kuwa  baada ya ukaguzi huo hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria zimechukuliwa ikiwemo kuwapatia Amri Tekelezi waajiri waliobainika kukiuka Sheria za kazi na baadhi ya wafanyakazi raia wa kigeni kufutiwa vibali vyao vya kazi.

Aidha serikali ilisemakuwa ya Waziri Mkuu itaendelea kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kuhakikisha maelekezo yanayotolewa yanazingatiwa ipasavyo na hivyo kumarisha mahusiano mema baina ya waajiri na wafanyakazi katika maeneo hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!