August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yapanga kudhibiti mazao yake

Spread the love
SERIKALI inapanga kuacha kusafirisha mazao yake nje ya nchi hususan yanapokuwa gafi, anaandika Happiness Lidwino.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa miaka mitano unaolenga kuunganisha minyoyroro minne ya  mazao  ambayo Pamba, Alzeti, Ngozi na jamii ya kunde, Dk. Adelhelm Meru, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji amesema kuwa, wanatarajia kuweka muungano wa pamoja kati ya mazao ya kilimo hadi yanapofika kiwandani ili kuepusha kuyapeleka nje ya nchi yakiwa gafi.
“Tumeunganika  hapa na watu kutoka International Trade Centre kwa ajili ya kuangalia namna ya kuwezesha Tanzania kupiga hatua kibiashara hususan katika mazao yake.
“Mara nyingi Tanzania kumekuwa na kutokulinganiswa kwa mazao ya kilimo pamoja na mazao yanayohitajika viwandani na hii ni kwakuwa mazao yanayozalishwa hayapewi kipaumbele.
“Tunaona kuna viwanda vinazalisha mafuta ya alzeti lakini Alzeti yenyewe haionekani, kuna viwanda vinazalisha ufuta lakini zao la ufuta halipo, hii ni kwa kua hakuna muunganiko mzuri, sasa tunatarajia mazao hayo manne kuachwa kupelekwa nje ya nchi,” amesema.
Amesema, kwa miaka mingi Tanzania imekuwa ikipata hasara kwa kupeleka mazao gafi nje hivyo kusababisha watu kukosa ajira na thamani ya zao kushuka.
“Tunawapelekea wenzetu machungwa kwa ajili ya kutengeneza juisi za maboksi na hatimaye wanakuja kutuuzia kwa bei ya juu, thamani ya mazao inapotea kwa sababu kama tungeshughulika na mazao yetu wenyewe, tungeweza kuzalisha na juisi ya boksi kupitia viwanda vyetu vyenyewe,” amesema.
Ringo Iringo, Mwenyekiti wa Chama cha Wasindika Mafuta ya Alzeti Tanzania (TASUPA) amesema kuwa, katika kipindi cha miaka mitano ijayo kutakuwa na mapinduzi makubwa kupitia  zao la Alzeti kutokana na zao hilo kuzalisha mafuta yanayopendwa nje ya nchi.
“Nchi kama India wanatumia mafuta ya Alzeti kwa asilimia 75 huku soko la ndani wakitumia mafuta ya alzeti kwa asilimia 60, na suala la  uzalishaji wa mafuta haya ni mkubwa ukilinganisha na mafuta ya kawaida,” amesema.
Iringo amesema,  licha ya zao hilo kuonekana kuwa nzuri lakini kumekuwa na sheria kandamizi kutoka kwa wakala wa Vipimo (WMA) ambao wamekuwa wakikandamiza sheria za upakiaji wa mazao kwa mfano wanahitaji gunia moja la alzeti kuwa na kilo 40, lakini bado kumekuwa na sheria kandamizi za kutoza mazao ya wakulima, na  kodi kupanda.
Emmanuel Mwangulumba, Ofisa Usimamizi Mkuu kutoka Bodi ya Pamba Tanzania  amesema, kwa upande wake zao la Pamba uzalishaji umepungua huku akiongeza kuwa hata Pamba inayozalishwa nchini imekuwa haina ubora kutokana na mbegu inayoendelea kutumika kuwa ni ya muda mrefu.
“Tunatarajia kufanya tafiti kuangalia mbegu bora ya pamba ambayo itaweza kuongeza uzalishaji wa pamba lakini pia kutoa pamba yenye ubora wa hali ya juu, sasahivi matumizi ya pamba nchini ni asilimia 30,” anasema.
Elibariki Mmari, mjumbe kutoka Sekta ya Ngozi ameiomba serikali iweka sheria ya kuimarisha viwanda vya ngozi ambavyo vitasaidia kuzalisha viatu vya ngozi.
error: Content is protected !!