Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yaonya waghushi vyeti chanjo ya Korona “tutaanza na watumishi”
Habari Mchanganyiko

Serikali yaonya waghushi vyeti chanjo ya Korona “tutaanza na watumishi”

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imeonya kwamba itachukua hatua kali,  dhidi ya watu watakaobainika kughushi vyeti vya chanjo ya Ugonjwa wa Korona (UVIKO-19). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Onyo hilo limetolewa leo Jumapili, tarehe 8 Agosti 2021 na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi, akitoa tathmini ya zoezi la chanjo hiyo, tangu lizinduliwe na Rais Samia Suluhu Hassan, tarehe 28 Julai mwaka huu.

“Serikali inatoa tahadhari iwapo kuna watu watakao jaribu kujipatia vyeti vya chanjo kwa njia za udanganyifu kuwa,  watabainishwa na mfumo na kuchukuliwa hatua za kisheria . Ikumbukwe kuwa,  wizara inafahamu mfuatano wa namba zake na zimetolewa kituo gani,” amesema Prof. Makubi.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi

Katibu mkuu huyo ameongeza ” hivyo ikitokea namba moja imejirudia, uchunguzi utaanza kwa watoa huduma waliotoa namba hizo na wateja wenye vyeti vya namba hizo  hivyo.”

Prof. Makubi amesema kuwa, Serikali inakamilisha mfumo wa kielektroniki wa vyeti vya chanjo hiyo.

“Serikali inaendelea kuboresha huduma za upatikanaji wa vyeti, kwa kukamilisha utaratibu wa kuhama kutoka mfumo wa vyeti vya makaratasi na kwenda kwenye mfumo wa vyeti vya kidigitali. Hivyo, naomba kuwahakikishia wananchi taarifa zote za usajili na vyeti kwa wale waliochanjwa, zimeandikwa katika vitabu na baadae taarifa hizo zitahamishwa katika mfumo wa kielektroniki,” amesema Prof. Makubi.

Prof. Makubi ametoa wito kwa watoa huduma za chanjo ya Korona,  kuwa waaminifu.

“Natoa wito kwa watoa huduma ya chanjo na wapokea huduma, kila mmoja kutimiza wajibu wake na kujiepusha na udanganyifu,” amesema Prof. Makubi.

Baada ya Rais Samia kuzindua zoezi la utoaji chanjo, huduma hiyo ilianza kutolewa rasmi kwa wananchi tarehe 3 Agosti mwaka huu.

Hadi jana Jumamosi, wananchi 105,745 walipata chanjo hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!