January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yaonya vituo vya malezi ya watoto

Watoti wa kituo cha Mwandaliwa Orphanage kilichopo Bunju wakipokea msaada kutoka PSPF

Spread the love

SERIKALI imesema kuwa, itaendelea kuvifungia vituo vyote vya kulelea watoto waishio katika mazingira magumu ambavyo vinaendeshwa kwa kukwepa taratibu na kanuni za uanzishwaji wake. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Steven Kebwe alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Sabrina Sungula (Chadema).

Katika swali la nyongeza la mbunge huyo, alitaka kujua ni kwanini serikali isitoe ruzuku kwa vituo ambavyo vinatoa malezi kwa watoto waishio kwenye mazingira magumu badala ya kuvifunga vituo hivyo.

“Kama serikali inasema kweli kuwa, ina uwezo wa kutoa ruzuku kwa vituo hivyo, ni kwa hatua gani sasa ambazo zimefanywa kwa lengo la kuvipatia ruzuku vituo hivyo ili visifungwe?

“Mbona sasa Kituo cha Onolatha kilichopo Jijini Dar es Salaam badala ya kukipatia ruzuku kituo hicho ambacho kimsingi kinafanya kazi ya kuisaidia serikali, kimefungwa” alihoji Sungura.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua ni kwanini serikali isiviwezeshe vituo vya kulelea watoto ili viweze kuwa na tija katika jamii.

Dk. Kebwe amesema, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inasimamia utoaji wa huduma katika watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi.

Na kuwa, kwa mujibu wa sheria ya mtoto Na. 21 ya mwaka 2009, kanuni 3(c) makao ya watoto ni suluhisho la mwisho kabisa katika kutoa malezi ya watoto na malezi hayo yanatakiwa yawe ya muda mfupi katika makao.

error: Content is protected !!