July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yaongeza siku 3, uandikishaji wapiga kura

Suleiman Jafo, Waziri wa Tamisemi

Spread the love

SERIKALI yaongeza siku tatu katika zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye Daftari la Orodha ya Wapiga Kura. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Zoezi hilo lililoanza tarehe 8 Oktoba 2019 na kutarajiwa kumalizika kesho, sasa litaendelea hadi tarehe 17 Oktoba mwaka huu.

Tangazo hilo limetolewa leo tarehe 13 Oktoba 2019 na Seleman Jaffo, Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Taarifa ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeeleza Jafo ametangaza kuongeza siku hizo, ili wananchi wapate fursa ya kujiandikisha.

“Waziri Jafo atangaza kuongeza siku Tatu za Uandikishaji wa Wapiga kura kwenye Daftari la Orodha ya Wapiga Kura; Sasa zoezi hilo litakamilika Tarehe 17/10/2019,” imeeleza taarifa hiyo.

 

error: Content is protected !!