May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yaongeza kima cha chini mshahara asilimia 23.3

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameridhia mapendekezo ya nyongeza ya mshahara kwa watumishi wa umma, ambapo kima cha chini kimeongezwa kwa asilimia 23.3. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus, leo Jumamosi, tarehe 14 Mei 2022, Serikali imepanga kutumia Sh. 9.7 katika mwaka wa fedha wa 2022/23, kwa ajili ya kugharamia mishahara ya watumishi wote katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na Wakala wa Serikali.

“Hivyo, bajeti ya mishahara ya mwaka 2022/23 ina ongezeko la Sh. 1.59 trilioni, sawa na asilimia 19.51, ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha wa 2021/22,” imesema taarifa ya Zuhura.

Taarifa ya Zuhura imeongeza kuwa, nyongeza hiyo imefanyika kwa kuzingatia pato la taifa (GDP), mapato ya ndani yanayotarajiwa kukusanywa katika mwaka 2022/23 na hali ya uchumi wa ndani na nje ya nchi.

Katika hatua nyingine, taarifa ya Zuhura imesema Rais Samia amepokea mapendekezo ya kanuni mpya ya Mafao ya Pensheni , yaliyotolewa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), katika sherehe za siku ya wafanyakazi duniani.

“Rais Samia ameridhia na kuilekeza wizara yenye dhamana na masuala ya hifadhi ya jamii kuendelea kushirikiana na TUCTA na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), ili kukamilisha taratatibu za kuhakikisha malipo ya mkupuo ya asilimia 25 yaliyokataliwa na wadau 2018, yanapandishwa hadi asilimia 33,” imesema taarifa ya Zuhura.

error: Content is protected !!