Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari Serikali yaombwa kupeleka wataalamu wa mifugo kwa wafugaji
Habari

Serikali yaombwa kupeleka wataalamu wa mifugo kwa wafugaji

Spread the love

 

SERIKALI imeombwa kuhakikisha inapeleka wataalamu wa mifugo kwa wafugaji ili kuweza kufanya ufugaji wenye tija. Anaripoti Danson Kaijage,Dodoma(Endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 29 Julai mwaka 2022 na Amoss Mwanyovellah ambaye ni moja wa wafugaji alipokuwa akizungumzia na waandishi wa habari juu ya ufugaji bora wa ng’ombe wa kisasa.

Mfugaji huyo amesema kuwa pamoja na kuwepo na changamoto mbalimbali lakini bado kuna tatizo la matibabu ya mifugo ikiwa ni gharama kubwa za kuipatia chanjo mifugo hiyo.

Akizungumzia upatikanaji wa maziwa amesema kuwa kutokana na matunzo bora ya ng’ombe wake anauhakika wa kupata lita za maziwa 30 kwa Ngombe mmoja kwa siku jambo ambalo amesema anajipatia kipato cha kutosha kupitia mifugo hiyo.

Mfugaji huyo amesema ufagaji wa mifugo ya kisasa kama vile Ng’ombe wanahitaji uangalizi makubwa ikiwa ni pamoja na kuwapatia matibabu ya mara kwa mara.

Aidha Mwanyovellah ameeleza kuwa pamoja na kuwepo kwa ufugaji wa ng’ombe wa kisasa bado kunachangamoto kubwa ya matibabu kutokakana na kuwepo kwa changamoto ya kukosekana kwa wataalamu wa matibabu kwa mifugo.

“Suala la matibabu kwa mifugo ni changamoto kuwa kwani unapokuwa na mifugo au unapokuwa na ng’ombe wenye thamani ya milioni tano na unahitaji mtaalamu wa tiba ya mifugo anaweza kuja mtaalamu na kujifanya kuwa mfugo una ugonjwa fulani kumbe siyo sawa.

“Kutokana na hali hiyo serikali naiomba iweze kusambaza zaidi wataalamu wa mifugo ili kuweza kutambua makundi ya wafugaji wa kisasa na kienyeji,”ameeleza mfugaji Huyo.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Maziwa ya Dodoma halisi, Anthony Msanga, amewataka wafugaji kuhakikisha wanafuga ufugaji wa kibiashara na wenye tija badala ya kufuga kwa mazoea.

Msanga amesema kuwa ufugaji wa kisasa utasaidia kuongezeka kwa upatikanaji wa maziwa jambo ambalo litasaidia mfugaji kujiongezea kipato lakini pia kuondoa udumavu wa watoto pamoja na watu wazima kwa kukosa virutubisho vinavyotokana na maziwa.

“Kwa mujibu wa maelezo ya afya juu ya utumiaji wa maziwa mtanzania anatakiwa kutumia lita 200 za maziwa kwa mwaka lakini watanzania wengi wanatumia kiwango cha chini cha maziwa
“Watanzania kwa sasa waatumia kiwango kidogo cha maziwa kati ya lita 60-64 kwa mwaka badala ya lita 200 kwa mwaka,” amesema Msanga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!