Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya Serikali yaokoa Bil 10 za chanjo
Afya

Serikali yaokoa Bil 10 za chanjo

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Spread the love

KUKAMILIKA kwa ujenzi wa jengo la Bohari ya Taifa ya chanjo, umesaidia kuokoa Sh. 10 bilioni kwa mwaka ambazo zingetumika katika kuhifadhi chanjo za watoto pamoja na vifaa. Anaripoti Hamisi Mguta …. (endelea). 

Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hiyo lililogharimu Sh. 1.2 bilion akiongozana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Zainab Chaula. 

Kwa kiasi kikubwa Waziri Ummy amesema ameridhishwa na hali ya ujenzi huo, hususan katika ujenzi wa vyumba vya kuhifadhia chanjo (stoo), jambo litalosaidia hasa wazazi wenye watoto wadogo kupata chanjo kwa wakati.

Pia,  Waziri Ummy amempongeza Meneja Mpango wa Taifa wa chanjo Dk.Dafrosa Lyimo kwa kushirikiana na Mkandarasi kwa usimamizi mzuri wa jengo hilo hadi kufikia hatua ya mwisho.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya Afya, Dk. Zainab Chaula ameahidi kuendelea kusimamia vizuri shughuli zote ili kuendelea kuboresha Sekta ya Afya kwa kasi ili wananchi wa hali zote wanufaike.

Kwa upande mwingine Dk. Zainab amesisitiza juu ya ushirikiano baina ya Watumishi katika Sekta ya Afya ili kurahisisha utendaji kazi kwa urahisi katika ngazi zote, hali itayosaidia wananchi kupata huduma bora.

Kwa upande wake Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo, Dk.Dafrosa Lyimo amesisitiza kwamba jengo hilo litakapokamilika litaleta faida nyingi katika kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo kurahisisha usambazaji wa chanjo katika ngazi ya mkoa na kurahisisha upatikanaji wa chanjo hizo katika ngazi zote kwa wakati wowote.

Dk. Lyimo ameahidi kuendelea kusimamia kwa ukaribu shughuli zote za mpango huo ikiwemo upatikanaji wa Chanjo kwa wakati wote na mahali popote ili wananchi waendelee kupata huduma hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

AfyaTangulizi

Wanasayansi wagundua teknolojia ya kunyofoa VVU kutoka kwenye seli

Spread the loveTIMU ya wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam cha nchini...

Afya

Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8

Spread the love  SERIKALI imetoa Sh 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi...

error: Content is protected !!