February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yanunua mashine 10 za X-ray

Spread the love

MASHINE kumi za mionzi (digital X-ray) zenye thamani ya Sh. 1.74 bilioni zimenunuliwa na serikali kwa ajili ya kuboresha huduma za afya nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mashine hizo zimepokelewa leo tarehe 2 Oktoba 2018 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kutoka katika Bohari ya Dawa (MSD) jijini Dar es Salaam.

Baada ya kupokea mashine hizo, Waziri Ummy amesema mashine hizo zitapelekwa kwenye hospitali za rufaa za mikoa 10 ambazo baadhi yake X-ray zilizokuwepo zimekwisha muda wake.

Hospitali hizo ni pamoja na Amana, Bukoba, Katavi, Morogoro, Njombe, Ruvuma, Simiyu na Singida pamoja na hospitali za Wilaya ya Magu na Nzega.

“Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania yataletwa na wananchi wenye afya na wenye uwezo wa kuzalisha mali,hivyo tunaboresha na kuimarisha huduma za tiba na uchunguzi wa magonjwa katika hospitali zetu kuwa na vifaa vya kisasa zaidi na kuondokana na utaratibu wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi,” amesema Waziri Mwalimu.

Waziri Ummy amesema Serikaki inaendelea kutoa kipaumbele katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwa ni lengo la kuhakikisha huduma za afya zinawafikia watanzainia wote karibu na maeneo wanayoishi.

error: Content is protected !!