Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yamliza Makonda, atoa laana
Habari za SiasaTangulizi

Serikali yamliza Makonda, atoa laana

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Spread the love

PAUL Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam yupo kwenye mtihani wa kunasua ‘makontena yake yaliyobeba samani’ bandarini jijini Dar es Salaam. Anaandika Yusuph Katimba … (endelea).

Samani hizo ni msaada uliotolewa na Watanzania wanaoishi Marekani wanaojulikana kwa jina la Six Region Diaspora Council.

Hata hivyo, wiki iliyopita taasisi ya serikali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilipiga mnada makontena hayo ambapo mteja hakupatikana kutokana na kudaiwa kuuzwa kwa bei kubwa (milioni 60) wakati wateja walioendekeza mwisho iwe milioni 30.

Gazeti moja limemnukuu Makonda akionesha  kulalamikia hatua ya TRA kupiga mnada makontena hayo.

Makonda ambaye yupo ngara alieleza kuwa, haridhishwi na hatua ya TRA kupiga mnada makontena hayo.

Makonda amenukuliwa akisema “amelaaniwa mtu yule atakaye nunua furniture (samani) za walimu. Nimefanya ibada maalumu leo (jana) ya kuhakikisha makontena hayo hayapati wateja kwa sababu naamini Mungu alinipa kwa ajili ya walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, wanaofanya kazi katika mazingira magumu ikiwa ni jitihada zangu binafsi.”

Makonda alieleza zaidi kuwa, katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli za kutoa elimu bure kwa Watanzania hasa watoto wa maskini, aliamua kuanzisha kampeni hiyo.

Alisema akiwa kama msaidizi wa Rais Magufuli katika mkoa huo:  “Sikuona sababu ya kukaa kimya wakati mazingira ya walimu siyo rafiki na kusubiri kuwalaumu walimu pale watoto wanapofeli bila kufanyia kazi changamoto zao.

“Leo TRA wameamua kuuza samani za walimu kwa wamiliki wa kumbi za starehe ili walimu waendelee kugombania madawati na vyoo na wanafunzi .  Mimi Paul Makonda nimefanya kwa sehemu yangu kilichobaki ni mwenye wazo atasimama siku moja kujitetea.”

Kontena hizo zaidi ya 20 zilipigwa mnada na Kampuni ya udalali ya Yono Action Mart, zilikuwa na samani aina ya meza, viti na mbao za kufundishia wanafunzi.

Zinapigwa mnada kutokana na kushindwa kulipiwa kodi ya Sh. bilioni 1.2 zinazodaiwa na TRA baada ya kuwasili nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!