Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Serikali yalaani askari aliyemtwanga makofi raia hospitali
Afya

Serikali yalaani askari aliyemtwanga makofi raia hospitali

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi
Spread the love

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeeleza kuumizwa na hatua ya askari wa ulinzi (SUMA – JKT) kumpiga ndugu wa mgonjwa aliyefika kumjulia hali mama yake. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli huyo imetolewa leo tarehe 24 Januari 2021, na Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Abel Makubi wakati akizungumza na mafisa habari wa wizara hiyo katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma.

Kitendo cha askari huyo kilifanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

“Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesikitishwa na inalaani sana kitendo hicho kilichofanywa na mlinzi wa SUMA – JKT,” amesema Prof. Makubi.

Akielezea juu ya tukio hilo Prof. Makubi amesema, tarehe 22 Januari 22, 2021, askari huyo alionekana akimpiga ndugu wa mgonjwa katika maeneo ya hospitali hiyo na kwamba, jambo hilo ni kinyume cha maadili na taratibu za kazi.

Aidha, Prof. Makubi amesema, wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kupitia Mkuu wa Wilaya, imeelekeza mlinzi huyo atolewe kwenye kituo hicho cha kazi na kurudishwa Makao Makuu ya Kanda ya jeshi hilo kwa ajili ya hatua za kinidhamu kulingana na taratibu za jeshi hilo.

Hata hivyo, Prof. Makubi ameeleza kuwa, Katibu Mkuu (Afya) Prof. Mabula Mchembe, ameelekeza kupata maelezo kutoka kwa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wa jinsi tukio hilo lilivotokea, mazingira yake na hatua zilizochukuliwa na uongozi wa hospitali hiyo.

Pia, ufanyike uchaguzi kama kulikuwa na uzembe wa utekelezaji wa mfumo na mwongozo wa utoaji huduma kwa mteja (customer care), ambao ulitolewa na wizara kwa vituo vyote vya kutolea huduma za afya, ili kuona kama kulikuwa na udhaifu mpaka tukio hili kutozuilika.

Amesisitiza baada ya uchunguzi huo, hatua stahiki zitachukuliwa.

Mbali na hayo, Prof. Makubi ametoa rai kwa wananchi kuwa watulivu wakati hatua zikiendelea kuchukuliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaMakala & Uchambuzi

Uongo, uzushi, tiba ya matende, ngiri maji

Spread the loveKUNA uongo na uzushi katika jamii kuhusu wanaume, wanawake na...

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye VVU, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Afya

Kambi ya matibabu ya kibingwa Ruangwa yaacha vilio, DC atoa ombi JAI

Spread the loveMKUU wa Wilaya ya Ruangwa, Hassan Ngoma amefunga rasmi kambi...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yatoa kauli wanaolala nje Hospitali ya Muhimbili

Spread the loveSERIKALI imesema inajipanga kushirikiana na sekta binafsi kujenga majengo yatakayosaidia...

error: Content is protected !!