Tuesday , 27 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yakubali hoja za Sugu kurekebisha Magereza
Habari za Siasa

Serikali yakubali hoja za Sugu kurekebisha Magereza

Spread the love

SERIKALI imekubali kuufanyia kazi ushauri uliotolewa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu,’ (Chadema) kuhusu uboreshaji wa jeshi la magereza nchini. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Mbilinyi alitoa ushauri huo leo bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa kueleza kuwa Jeshi la Magereza lina hali mbaya ya vitendea kazi ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa magari ya kuwapelekea wahutumiwa mahakamani jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa watuhumiwa na askari.

“Mheshimiwa Spika licha ya kuwa magari katika hii Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Magereza halina magari kabisa hata mabovu hayapo jambo ambalo linawalazimisha askari magereza kuwafunga pingu wafungwa na watuhumiwa na kutembea nao kwa miguu mitaani.

“Jambo hili ni hatari matharani mtu anatuhumiwa mauaji halafu anatembezwa mitaani anaweza kuvamiwa na kupigwa na wananchi lakini pia ni hatari kwa askati magereza kwani anaweza kuvamiwa na kupigwa kutokana na hali hiyo nashauri serikali kuhakikisha mnaboresha Jeshi la Magereza kwa kulipatia vitendea kazi,” amesema Mbilinyi.

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum, Sikudhani Chikambo (CCM) alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kupeleka magari katika vituo vya polisi nchini.

Pia mbunge huyo alitaka kujua ni lini serikali itapeleka pesa kwenye vituo hivyo kwa ajili ya matengenezo ya magari na mafuta ya hayo magari ili polisi waweze kufanya kazi zao kwa uhakika.

“Kuna upungufu wa magari katika vituo vya polisi mkoa wa Ruvuma na hayo yaliyopo sasa ni mabovu na hayafanyiwi matengenezo kutokana na ukosefu wa fedha.

“Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka magari katika vituo vya polisi nchini, Je ni lini serikali itapeleka pesa kwenye vituo hivyo kwa ajili ya matengenezo ya magari na mafuta ya hayo magari ili polisi waweze kufanya kazi zao kwa uhakika,” aliuliza Chikambo.

Kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ajajibu maswali hayo Spika wa Bunge Job Ndugai alimpongeza Mbilinyi kwa kutetea Jeshi la Magereza kwa uzoefu alioupata.

Hata hivyo Mwigulu amesema kuwa kutokana na ushauri uliotolewa na Mbilinyi serikali itaufanyia kazi ili kuona ni jinsi gani ya kuwapatia magari ili kuepukana na askari magereza kutembea na wafungwa au mahabusu kwa kwa miguu.

Aidha Mwigulu amesema kuwa ni kweli magari mengi kwa sasa yamekuwa ni ya muda mrefu na yanahitaji matengenezo ya mara kwa mara ambapo jeshi la polisi linahitaji kufanya matengenezo kwa magari yaliyoharibika kwa kutumia fedha zinazopelekwa na kuwashirikisha wadau wa ulinzi na usalama .

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!