May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yakopa WB, IMF kukabili mfumuko wa bei

January Makamba, Waziri wa Nishati

Spread the love

 

SERIKALI imesema imeanza mchakato wa kuchukua mkopo kutoka Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa ajili ya kuwekaahueni kwenye bei za mafuta na bidhaa nyinginezo “zinazogusa maisha ya Watanzania.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Jumanne tarehe 10 Mei 2022, na Waziri wa Nishati, Januari Makamba wakati akiwasilisha bungeni taarifa ya Serikali kuhusu hatua za dharura za kukabili upandaji wa bei ya mafuta uliosababisha gharama za maisha kuongezeka.

Waziri huyo ameweka wazi kuwa mchakato wa kuchukua mkopo huo uko mbioni kukamilika na ahueni kwenye kupanda kwa bei za bidhaa itapatikana katika mwaka ujao wa fedha.

Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha inadhibiti mfumuko wa bei ikiwemo kupunguza tozo zenye jumla ya Sh 102 bilioni kwenye nishati ya mafuta.

Hata hivyo bei ya bidhaa hiyo imeendelea kupanda kwa kasi katika soko la dunia na kusababisha bei za mafuta hapa nchini kuongezeka kwa kiwango kikubwa mwezi Mei 2022 na kufikia Sh. 3,148 kwa lita ya petroli, Sh. 3,258 kwa lita ya dizeli na Sh. 3,112 kwa lita ya mafuta ya taa.

Bei hiyo imesababisha kupanda kwa nauli za daladala na mabasi ya mikoani na kuchochea kupanda kwa bidhaa zingine muhimu ikiwemo vyakula na vifaa vya ujenzi.

error: Content is protected !!