January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yakiri uhaba wa nguo za wafungwa

Wafungwa wakiwa katika shughuli zao za kawaida

Spread the love

SERIKALI imekiri kuwa, wafungwa wengi hawana nguo za kutosha kutokana na serikali kutokuwa na fedha za kutosha. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereila Ame Silima, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum, Kidawa Hamid Saleh (CCM).

Kidawa alitaka kujua ni kwanini wafungwa wengi wanakosa nguo na kulazimika kuvaa ambazo zimechakaa na zenye kuonesha miili yao.

Pia alitaka kujua ni mikoa gani au majiji ambayo yanaongoza kwa kuwa na wafungwa wengi kutokana na makosa mbalimbali.

Akijibu maswali hayo, Silima amesema ni kweli wafungwa wanakabiliwa na uhaba wa nguo lakini sio kweli kuwa wapo ambao wanashindwa kufanya kazi za nje kutokana na kuvaa nguo ambazo zinaonesha miili yao.

Aliutaja mkoa wa Tabora kuwa unaongoza kwa kuwa na wafungwa wengi ukifuatiwa na Tanga na Arusha.

Aidha, amesema kuwa Tanzania ina jumla ya magereza 126 yenye uwezo wa kulaza wafungwa na mahabusu 38,000 kwa siku, yakiwa yamegawanyika kwa makubwa 12, ya wilaya 68 na ya kilimo 46.

Silima amesema kuwa, wafungwa wanaotumikia vifungo mbalimbali katika magereza yote nchini kwa makosa ya ubakaji na udhalilishaji wa watoto na wanawake ni 1,067.

error: Content is protected !!