January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yakiri kutopandisha walimu vyeo

Maandamano ya Walimu wa mkoa wa Dar es Salaam

Spread the love

SERIKALI imekiri wazi kwamba walimu wengi hawapandishwi vyeo pamoja na kulipwa malimbikizo yao kwa wakati. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa leo bungeni na Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Majaliwa, alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kishapu (CCM) Suleman Nchambi.

Katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mikakati gani ya kuboresha maslahi ya walimu pamoja na kuwapatia vitendea kazi.

“Walimu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchelewa kupandishwa madaraja, kuchelewa kupatiwa malimbikizo ya madeni yao pamoja na kukosekana kwa vitendea kazi kama kipaumbele.

“Je serikali ina mikakati gani ya kuhakikisha inawafanikishia walimu hao kama sehemu ya kipaumbele kwa walimu hao” alihoji mbunge.

Akijibu swali hilo Majaliwa alisema ni kweli walimu wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali kama zilivyotajwa na mbunge.

Amesema licha ya kuwepo kwa changamoto hizo serikali inaendelea na mikakati ya kuwawezesha walimu kufanya kazi katika mazingira rafiki.

Amesema serikali imeweka mikakati ya kuboresha maslahi ya walimu nchi nzima, ikiwa ni pamoja na kuboresha makazi kwa maana ya kuwajengea nyumba walimu.

Amesema katika 2009 hadi mwaka 2013 serikali imetoa shilingi bilioni 13.9 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu ikiwemo shilingi milioni 148.6 zilizopelekwa halmashauri ya wilaya ya kishapu.

error: Content is protected !!