January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yakiri ahadi za Kikwete kutokamilika

Rais Jakaya Kikwete

Spread the love

SERIKALI imekiri kuwepo kwa ahadi nyingi za Rais Jakaya Kikwete ambazo hazijakamilika mpaka sasa. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Hata hivyo serikali imesema, inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha ahadi hizo zinakamilika kabla ya kuondoka kwake madarakani.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Biharamulo Magharaibi, Dk.Antony Mbassa (Chadema).

Katika swali la nyongeza Dk. Mbassa alitaka kujua, ni lini ahadi ya Rais Kikwete ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege uliopo katika Wilaya ya Biharamulo itatekelezwa.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo, alitaka kujua serikali ina jitihada gani za kukarabati Kiwanja cha Ndege ikiwa ni pamoja na kuongeza eneo la kurukia ndege ili kuwezesha ndege kubwa zaidi kutua katika kiwanja hicho.

“Kiwanja cha Ndege kilichopo Biharamulo kinachohudumia Wilaya ya Biharamulo, Chato, Muleba Kusini, Ngara na Buyugu una eneo fupi la kuruka na kutua ndege meta.

“Je, serikali ina jitihada gani za kukarabati Kiwanja cha Ndege ikiwa ni pamoja na kuongeza eneo la kurukia ndege ili kuwezesha ndege kubwa zaidi kutua katika kiwanja hicho na huduma za zima moto zikoje katika kiwanja hicho?” amehoji Dk. Mbassa.

Akijibu swali hilo Dk. Tizeba amesema, serikali ina nia ya dhati ya kuviboresha viwanja vyote vya ndege vyenye barabara za kuruka na kutua ndege za changarawe na nyasi.

Amesema, viwanja hivyo ni pamoja na Kiwanja cha Ndege cha Biharamulo ambapo katika mpango wa muda mrefu, wizara kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) itaendelea na juhudi za kuboresha miundombinu ya viwanja vyote vya ndege nchini kulingana na upatikanaji wa fedha.

error: Content is protected !!