January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yajipanga kudhibiti kemikali

Spread the love

SERIKALI imeandaa mkakati wa udhibiti wa kuingia kemikali hatari zenye madhara kwa afya ya binadamu kwenye maeneo ya bandari. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samweli Manyele amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuwa ofisi yake imeandaa mafunzo ya siku moja kukabiliana na kemikali hatarishi.

Profesa Manyele amesema kuwa wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali imetayarisha mwongozo wa utendaji wa kazi wa wadau wa bandari ambapo mwongozo huo utasambazwa kwa wadau hao kabla ya kutumika ili kubereshwa kupitia maoni yao, wadau hao ni mamlaka ya bandari za bahari na mipaka inayotumika kuingiza na kutoa bidhaa mbalimbali.

Ametaja kiwango cha kemikali zilizoingia nchini kwa kipindi cha Januari hadi Oktoba mwaka huu ni tani 472,393 ambapo bandari ya Dar es Salaam imekuwa inaingiza kiwango kikubwa cha kemikali kuliko bandari na mipaka mingine ambapo imefikia tani 281,468 asilimia 59.6 ambapo mpaka wa Mtambaswala kiasi kidogo cha kemikali kufikia tani 506.00 sawa asilimia 0.1.

Profesa Manyele amesema kuwa hatua kadhaa zitazochukuliwa ni pamoja na kukuza mahusiano ya nchi za Afrika Mashariki, warsha kwa wakuu wa usalama wa barabarani na wadau wa bandari.

error: Content is protected !!