July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yajiondoa ulipaji wa makocha

Spread the love

SERIKALI imesema haitaweza kumlipa kocha yoyote nchini na badala yake wataviwezesha vyama vya michezo kuwa na uwezo wa kulipa garama hizo. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanii na Michezo, Nape Nnauye, alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufungua mbio za Chama cha Riadha Tanzania (RT).

Mbio hizo zilizotawaliwa na Kaulimbiu ya “Dodoma hapa kazi tu Half Marathoni” zilizinduliwa na Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa huku zikiwa chini ya udhamini wa GSM Foundation, Kadco, NHC na Kilimanjaro, Aloe Vera.

Nape alisema ni wajibu wa serikali kusaidia vyama vya michezo nchini na kuviwezesha kuwa na uwezo wa kuwagarimikia makocha wao wenyewe kulingana na mahitaji yao.

“Umefika wakati kama wadau wa michezo kubadilika na kuanza kuwekeza katika michezo mingine kama riadha badala ya kuwekeza katika mpira wa miguu peke.”

Alisema serilikali inalenga kuhakikisha michezo inakuwa sehemu ya ajira badala ya kuwa na sura ya Burudani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Olimpiki (TOC), Fribert Bayi alisema chama hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi zinazo hitaji utatuzi wa pamoja.

“Tunahitaji kuwekeza nguvu zetu zote kwa pamoja kama tunahitaji kupiga hatua za kusonga mbele kufikia waliko wenzetu” amesema Bayi.

Amesema kama tunataka kupata wachezaji wazuri ni hatuna budi kuwaandaa watoto wangali wakiwa na umri mdogo.

Amesema kwa sasa hapa nchini wapo wachezaji wawili tu ambao wana sifa ya kushirika michezo ya Olimpiki huku wengine kumi wakiwa katika makambi kwa lengo la kujifua kuweza kufikia kiwango.

error: Content is protected !!