July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yajikanyaga umeme vijijini

Mafundi umeme wakiwa kazini

Spread the love

SERIKALI imejigamba itaendelea kutekeleza ahadi yake ya kupeleka nishati ya umeme vijijini. Charles Mwaijage, naibu waziri wa nishati na madini, ameliambia bunge mjini Dodoma, kuwa serikali inaendelea kukarabati njia za umeme katika wilaya zote nchini. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Mwijage alikuwa akijibu swali lililoulizwa na mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR- Mageuzi), Moses Machali. 

Katika swali lake la msingi, Machali alitaka kujua kama serikali haioni umuhimu kukarabati nyaya, mita na vifaa vingine ili kuhakikisha umeme takribani megawati 2 hazipotei kama ilivyo sasa.

Machali alitaka kufahamu utekelezaji wa ahadi ya serikali iliyotoa bungeni katika mkutano wa bajeti wa mwaka 2013 ambako iliahidi kusambaza umeme katika vijiji vya Nyumbigwa, Murufiti, Kidyama, Herujuu Mganza, Ruhita na Kanazi. 

Mwijage amesema vifaa vya kujenga miundombinu ya umeme vilivyoagizwa kutoka nje ya nchi na vinaendelea kupelekwa Kasulu ambapo wateja wanaendelea kuunganishiwa umeme.

Amesema  umeme unaozalishwa haupotei kama ilivyokuwa hapo awali baada ya wateja 4,400 kuunganishiwa umeme hivyo kufanya wateja 4,700 kunufaika na huduma ya umeme kwa sasa kutoka wateja 300 mwaka 2011.

error: Content is protected !!