August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yajibu mapigo ya Mbowe

Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO,Hassan Abbasi

Spread the love

HATIMAYE  hoja zilizotolewa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) zimemuibua msemaji wa serikali wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Hassan Abbas, anaandika Catherine Kayombo.

Abbas ameibuka leo mchana na kusisitiza kwamba uchumi wa Tanzania bado uko imara tofauti na ilivyosemwa na Chadema kupitia mwenyekiti wake Freeman Mbowe, alipokutana na wanahabari kueleza maazimio ya kikao cha kamati kuu ya chama hicho  kilichofanyika tarehe 29-30 Julai jijini Dar es Salaam.

Mbowe aliyataja maeneo yanayoyumbisha uchumi wa nchi kuwa ni pamoja na mwenendo wa mikopo katika sekta binafsi, ongezeko la deni la taifa na kushuka kwa mzunguko wa fedha kusababisha kuathiri biashara.

Akizungumza na wanahabari, Abbas amesema, uchumi wa upo vizuri ukilinganisha mataifa mengine barani Afrika, kwa miaka mitatu mfululizo bado uko katika ukuaji usiopungua asilimia 7.0 hadi 7.2.

Amesema ukuaji wa uchumi unaizidi Rwanda ambayo inakua kwa  6%, Uganda 5% na Kenya 6.4%.

Amesisitiza kuwa uimara wa uchumi wa nchi ni namna ya  kudhibitiwa kwa mfumuko wa bei, kuendelea kuvutia uwekezaji na utekelezaji wa miradi mikubwa.

Amewataka wananchi kuchapa kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo bila kutegemea nguvu ya serikali.

 

 

 

 

error: Content is protected !!