Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yaja na waratibu wa umeme vijijini kila jimbo
Habari za Siasa

Serikali yaja na waratibu wa umeme vijijini kila jimbo

Spread the love

 

KATIKA kuimarisha usimamizi wa miradi ya kupeleka umeme vijini, Serikali imesema inakwenda kuajiri waratibu wa miradi ya umeme vijijini kwa kila jimbo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Jumatano tarehe 1 Juni, 2022 na Waziri wa Nishati, Januari Makamba, akiwasilisha bajeti yam waka 2022/2023.

Mbali na kuimarisha usimamizi wa miradi Makamba amesema pia Waratibu watarahisisha upatikani wa taarifa za maendeleo ya miradi hiyo.

“Waratibu hao watakuwa kiungo cha mawasiliano na taarifa kati ya Wabunge, viongozi wa kisiasa, wakandarasi, REA na wadau wengine,” amesema Makamba.

Ameongeza kwa kushirikiana na TANESCO, waratibu hao watakuwa na wajibu wa kutoa taarifa za mara kwa mara kwa viongozi ikiwemo wa Wabunge kuhusu maendeleo ya miradi.

January Makamba, Waziri wa Nishati

Katika hatua nyingine Makamba amesema Serikali imesikia kilio cha muda mrefu cha wananchi wanaoishi katika maeneo ya mijini yenye sifa zinazolingana na vijiji huku wakilipa bei ya kuunganishiwa umeme ya mijini.

“Nataka niwahakikishie kwamba tumesikia kilio chao na tayari tumeunda timu inayojumuisha Wizara ya Nishati, TANESCO na REA.

“Timu hii itazunguka katika miji yote na kuyabaini maeneo hayo kwa kuwashirikisha Waheshimiwa Wabunge wa maeneo husika.

Amesema maeneo yatakayobainishwa na timu hiyo yatajumuishwa kwenye bei ya vijiji yaani Sh. 27,000, “zoezi hili litafanyika nchi nzima na kukamilishwa ndani ya miezi sita.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Biswalo aendelea kung’ang’aniwa fedha za ‘Plea Bargaining’, CUF wataka ajiuzulu

Spread the love  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka...

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

error: Content is protected !!