Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yaja na mikakati 7 kuwezesha wananchi kiuchumi
Habari za Siasa

Serikali yaja na mikakati 7 kuwezesha wananchi kiuchumi

Spread the love

SERIKALI imetoa maagizo saba kwa viongozi, Asasi za Kiraia na kijamii, wadau wa maendeleo na mashirika ya kimataifa, yenye lengo la kuchagiza masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Maagizo hayo yametolewa leo tarehe 15 Juni 2019 na Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wakati akifungua Kongamano la Nne la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Jijini Dodoma.

Waziri Majaliwa amesema mamlaka za serikali, wadau wa maendeleo, mashirika ya kimataifa na asasi za kijamii na kiraia, zinatakiwa kutekeleza maagizo hayo ndani ya mwaka mmoja, na kwamba katika kongamano la mwaka ujao, kila taasisi itawasilisha ripoti ya utekelezwaji wake.

“Mifukoya sekta binafsi iendelee kuimarishwa na kufuatilia utendaji wao, tunachotaka hii dhana ya uwezeshaji wananchi kiuchumi lazima iwafikie, kwa kufanya hilo tutaanza kuona wananchi wakifurahia uwepo wa taasisi zinazotoa mitaji kwa wajasiriamali,” amesema Waziri Majaliwa

Miongoni mwa maagizo hayo ni  mikoa na halmashauri zote nchini kuanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili kuharakisha nia ya serikali katika kuwezesha wananchi kiuchumi.

“Na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi liandae na kusimamia utekelezaji  wa muongozo utakaotumika kuanzisha vituo vya namna hiyo kote nchini,”ameagiza Waziri Majaliwa.

Agizo lingine ni mikoa isiyokamilisha muongozo wa uwekezaji ihakikishe inakamilisha suala hilo ndani ya mwaka mmoja, na kwamba kipindi hicho kikimalizika serikali itapima utekelezaji wa gizo hilo.

Waziri Majaliwa ameagiza mikoa yote iliyokamilisha kuandaa muongozo wa uwekezaji sambamba na kuonesha utekelezaji katika kutumia fursa mbalimbali zilizoainishwa pamoja na mikakati ya kutangaza fursa hizo kwenye maeneo yao.

Sambamba na hayo, Waziri Majaliwa ameagiza uboreshwaji wa mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili ifikie Watanzania wengi hususan maeneo ya vijijini.

“Saba, mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi iboreshwe sambamba na kuongeza ufanisi ili ifikie Watanzania wengi hususan vijijini, kamilisheni na zindueni haraka mfumo wa kupima matokeo ya kiuchumi na si shughuli wanazofanya,” ameagiza Waziri Majaliwa.

Hali kadhalika, Waziri Majaliwa ameliagiza Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuratibu mifuko ya uwezeshaji ,ikiwemo ya serikali na sekta binafsi iliyopo, pamoja na kufuatilia utendaji kazi wake ikiwemo namna gani inafikia wananchi.

“Pia, tumetoa maelekezo kwa serikali kazi hii tumewapa baraza waratibu mifuko yote ya uwezeshaji nchini , ya sekta binafsi na serikali.  tuitambue iko mingapi,  inafanya nini na nani mnufaika.  Je wanufaika wanajitambua,” amesema Waziri Majaliwa na kuongeza.

“Ili baadae serikali ifanye maamuzi ya kubaki na mifuko yote hiyo au tuinganishe tupate michache inayoweza kuratibiwa vizuri ili itoe matokeo.”

Aidha, Waziri Majaliwa ameagiza wadau wa maendeleo kuwasilisha taarifa za utekelezaji wao kwenye ofisi yake ili ziweze kuisaidia serikali katika kuweka mipango ya kuwezesha wananchi kiuchumi.

“Kila mdau wa uwezeshaji ahakikishe kuwa,  anawasilisha taarifa hizo ofisi ya waziri mkuu kupitia baraza letu la uwezeshaji wananchi kiuchumi.  Ili ziweze kusaidia katika kuweka mipango iliyoko na ile mikubwa iliyoko ndani ya serikali,” amesema Waziri Majaliwa na kuongeza.

“Serikali inatambua na kuthamini mchango wa wadau wa maendeleo, mashirika ya kimataifa, asasi za kiraia na sekta binafsi ambao kimsingi wanafanya kazi kwa niaba ya serikali. Hivyo taarifa zenu ni muhimu sana.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

error: Content is protected !!