August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yaja na mifumo mipya kupima utendaji kazi wa watumishi

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi

Spread the love

 

SERIKALI imesema mara baada ya kukamilisha mifumo mipya ya kupima utendaji kazi wa watumishi wa umma, itapeleka bungeni Muswada wa Sheria uweze kupitishwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa bungeni leo Jumatano tarehe 29 Juni, 2022 na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi, wakati akijibu swali na Mbunge wa Mlimba, Godwin Kunambi kutaka kujua ni lini Serikali itapeleka bungeni Muswada wa kubadili Sheria ya Utumishi wa Umma na kubadili mfumo wa OPRAS.

Ndejembi amesema Rais Samia amekuwa akizungumzia mabadiliko ya mfumo wa kupima utendaji kazi wa watumishi wa umma tangu siku ya kwanza akilihutubia Bunge Aprili 2021.

Amesema tayari imefanya mapitio ya mfumo wa OPRAS na kufanya usanifu wa mifumo mipya na inakaribia kukamilisha ujeni wa mifumo mipya miwili ikiwemo mfumo wa usimamizi wa utendaji kazi wa taasisi za umma PIPMIS na mfumo wa usimamizi wa utendaji kazi wa watumishi wa umma PEPMIS.

“Mifumo hii itaanza kazi haraka katika mwaka wa fedha 2022/2023,” amesema.
Ndejembi amemshukuru Rais Samia Syulhu Hassan kwa miongozo na maelekezo yake katika jambo hilo la usimamizi wa utendaji kazi wa watumishi wa umma na taasisi za Serikali.

“Wote hapa ni mashuhuda mwaka jana Aprili alitaja mabadiliko ya mfumo wa OPRAS na amekuwa akilizungumzia suala hili kwenye vikao vyote. Nikuhakikishie tunaleta mabadiliko makubwa sana katika upimaji wa utendaji wa watunmishi wa umma na mifumo hii ikishakamilika ya PEPMIS NA PIPMIS tutaleta muswada hapa bungeni ili kuleta mabadiliko na wabunge mpitishe tuanze kuwapima watumishi wetu,” amesema.

Akijibu swali la nyongeza la Kunambi akitaka kujua ni ipi kai ya mifumo hiyo itakayo kwenda kupima vuongozi wa kisera ambao waliachwa kwenye mfumo wa OPRAS, Ndejembi amesema kwa upande wa mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya utendaji kazi wao unapimwa na mamlaka ya uteuzi huku Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Wakuu na Ma-RAS huwa wanasaini mkataba wa utendaji na Katibu Mkuu Kiongozi.

error: Content is protected !!