December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yaja na hati maalumu mbadala wa uraia pacha

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula

Spread the love

 

WAZIRI ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Leberata Mulamula amesema kwa sasa Serikali inaandaa mchakato wa kuwa na hati maalumu ili kukidhi mahitaji ya uraia pacha. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Balozi Mulamula amesema hayo jana tarehe 20  Novemba, 2021 wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua nini msimamo wa serikali kuhusu suala la uraia pacha.

Amesema pamoja na uhitaji wa uraia pacha lakini serikali inafanya mchakato wa kuwa na hati maalumu jambo ambalo amesema ni rahisi na linawezekana.

Amesema mchakato wa uraia pacha ni mlolongo mrefu lakini kuwa na hati maalum ni jambo ambalo linazungumzika kwa wepesi kwa sababu baadhi ya nchi wanatumia utaratibu huo.

Balozi Mulamula ambaye alikuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ikiwa ni utaratibu wa kila wizara kuelezea mafanikio kwa kipindi cha miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika na sasa Tanzania bara.

Passport ya Tanzania

Aidha, Balozi Mulamula amesema tangu kupatikana Uhuru, Tanzania imepiga hatua kutoka kuwa na mabalozi wawili mwaka 1961  hadi mabalozi 44 sasa.

Akizungumzia hatua ya nchi ya Denmark kufunga ubalozi wake hapa nchini Agosti mwaka huu, Balozi Mulamula amesema huo ni utaratibu wa kawaida kwani Tanzania haijafunga uhusiano na nchi hiyo

“Tanzania hatujapata shida yoyote kutokana na kufungwa kwa ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini na kwenda nchi jirani. Lakini pia ubalozi huo sio kwamba tumefunga mahusiano.

“Na ikumbukwe kuwa ubalozi huo umekuwa ukisaidia katika nchi zenye migogoro na Tanzania hatuna migogoro hivyo bado tupo salama na hatujaathirika na jambo lolote” amesema Balozi Mulamula.

error: Content is protected !!