Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yaipa H/shauri Hanang usimamizi shamba la ngano
Habari Mchanganyiko

Serikali yaipa H/shauri Hanang usimamizi shamba la ngano

Spread the love

 

SERIKALI imeikabidhi Halmashauri ya wilaya ya Hanang usimamizi na uangalizi wa muda wa mali zote zilizopo katika shamba la ngano la Basotu wilayani humo lenye ukubwa wa hekta 5,138 wakati Serikali ikiandaa mipango ya muda mrefu ya matumizi ya shamba hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara …  (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya mali katika shamba hilo kuwa chini ya uangalizi wa Mfilisi, Kampuni ya Uwakili ya Tadayo kwa zaidi ya miaka 15.

Mwaka 2004, Mfilisi, Wakili Joseph Tadayo ambaye pia ni Mbunge Mwanga (CCM) alikabidhiwa kwa ajili ya kuuza shamba na mali zake, lakini baadaye mwaka 2007, Serikali ilisitisha uamuzi huo na kuziacha mali hizo chini ya uagalizi wa Kampuni ya Uwakili ya Tadayo.

Aidha, Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto jana tarehe 16 Novemba, 2021 alipokea mali za shamba hilo la Basotu kutoka kwa Mfilisi, Wakili Joseph Tadayo, makabidhiano yaliyofanyika katika Ofisi za Msajili wa Hazina, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam, Benedicto aliishukuru Kampuni ya Tadayo kwa uangalizi iliyoufanya licha ya kuwepo kwa changamoyo mbalimbali.

Alisema hati hizo zinaonesha kuwepo kwa mali mbalimbali katika shamba hilo zikijumuisha mitambo na majengo 37, zikiwemo nyumba za makazi 28, maghala mawili, vihenge (silos) sita, ukumbi wa starehe, mgahawa, kanisa, duka na mitambo mbalimbali pamoja na matrekta na mashine za kuvunia nafaka.

Baada ya kukabidhiwa hati za mali ya shamba hilo, Mgonya alizikabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hanang, Jenifa Omolo kwa ajili ya uangalizi wa muda wakati serikali ikamilisha mpango wa matumizi wa muda mrefu wa shamba hilo.

“Tunaushukuru uongozi wa Halmashauri ya Hanang kwa ushirikiano mkubwa na sasa tunaiongezea jukumu lingine la uangalizi wa mali mpaka hapo maelekezo mengine ya Serikali yatakapotolewa,” alisema Benedicto huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hanang akiahidi kutimiza wajibu wake ili kulinda mali hizo za Serikali.

Naye Wakili Tadayo aliyekuwa Mfilisi wa Shamba la Basotu, alielezea kufurahia kukabidhi mali hizo, baada ya kuwa mwangalizi kwa muda mrefu, huku akikabiliana na changamoto kadhaa.

Shamba la Basotu ni kati ya mashamba saba ya ngano ya Serikali wilayani Hanang yaliyokuwa chini ya Shirika la Taifa la Kilimo na Chakula (NAFCO).

Aidha, ni shamba pekee ambalo halikubinafsishwa baada ya Serikali kusitisha uamuzi huo mwaka 2007.

Baada ya kukaa muda mrefu bila kubinafsishwa, kuliibuka vitendo vya uvamizi kutoka kwa wakulima na wafugaji wa maeneo jirani, hali iliyoilazimu Halmashauri kuiomba Ofisi ya Msajili wa Hazina iridhie shamba hilo liwekwe chini ya usimamizi wao ili kuzuia vitendo vya uvamizi wa shamba na wizi wa mali.

Mashamba mengine ni Gawal, Warret, Gidagamowd, Satchet, Murjanda na Mulbadaw.

Mashamba ya Gawal na Warret yalikabidhiwa kwa Halmashauri ya wilaya na kugawiwa wananchi kwa matumizi ya kilimo, ufugaji na makazi wakati mashamba ya Gidagamowd, Satchet na Murjanda yalibinafsishwa kwa Kampuni ya Ngano Limited mwaka 2005.

Shamba la Mulbadaw liliuzwa kwa Haydom Lutheran Hospital mwaka 2006.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!