July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yahimiza NHIF

Spread the love

SERIKALI imezitaka Hospitali za Serikali kutowapuuza wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya (NHIF) kwani ni chanzo kikubwa na uhakika cha mapato kwa hospitali hizo, anandika Dany Tibasoni, Dodoma.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Seleman Jafo, Naibu Waziri wa TAMISEMI, alipofanya ziara katika hospitali ya Makole katika Manispaa ya Dodoma.

Jafo amesema watumishi walio wengi ni wanachama wa Mfuko wa Bima ya Afya lakini bado hospitali za serikali zimekuwa maskini kimapato kutokana na kutowahudumia vizuri kuliko wale wanaolipa fedha taslimu.

Amesema mara nyingi wagonjwa wanakuwa na kadi hizo wamekuwa wakiacha kutumia hospitali hizo za serikali na kukimbilia za watu binafsi.

“Hakuna mtumishi ambaye si mwanachama wa mfuko huo lakini inaonekana hamuwatumii ipasavyo kama ilivyo kwa hospitali za watu binafsi,’’ amesema.

Ameongeza kuwa hata pale wanapowapa huduma mara nyingi wamekuwa wakiwaandikia cheti na kwenda kuchukua dawa kwenye maduka binafsi jambo ambalo ni kukimbiza mapato.

“Mtu akija hapa akiwa na kadi yake basi haudumiwe kwa haraka na dawa ziwepo siyo mnalalamikia vitendea kazi tu huku wateja walio wengine,” amesema Jafo.

Akitoa taarifa ya hospitali hiyo Dk. James Charles, Mganga wa Manispaa ya Dodoma, amesema hospitali hiyo ina upungufu wa vyumba vya kutolea huduma kwa sasa.

Amesema hali hiyo inatokana na hospitali hiyo kutumika kama hospitali ya wilaya jambo ambalo halikuwepo hapo awali.

Kwa mujibu wa Dk. James, kwa siku hospitali hiyo inapokea kati ya wagonjwa 350 hadi 400.

error: Content is protected !!