Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yagongelea msumari sakata la wamachinga
Habari Mchanganyiko

Serikali yagongelea msumari sakata la wamachinga

Spread the love

 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ummy Mwalimu, ameziagiza halmashauri kupanga miji upya, ikiwemo kuwaondoa wafanyabiashara wadogo ‘wamachinga’, katika maeneo yasiyo rasmi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo Jumamosi, tarehe 6 Novemba 2021, alipotembelea Soko la Kariakoo, lililopo jijini Dar es Salaam.

Waziri Ummy ameziagiza halmashauri hizo, kuwapeleka wafanyabiashara katika maeneo yaliyoandaliwa kwa ajili ya kufanya biashara.

Aidha, Waziri Ummy ameupongeza Mkoa wa Dar es Salaam, kwa kuwapanga wamachinga katika maeneo yaliyo rasmi.

“Lazima miji ipangwe vizuri na Rais Samia Suluhu Hassan, amesisitiza miji ipangwe na iwe salama. Changamoto hazikosekani lakini tuzitatue na naupongeza Mkoa wa Dar es Salaam kwa jitihada kubwa za kuwapanga wamachinga,” amesema Waziri Ummy.

Ummy amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe, akutane na maafisa mipango miji hao, ili waweke mikakati ya kuipanga miji vizuri.

Ummy Mwalimu

“Nimemuelekeza Katibu Mkuu TAMISEMI, tutawaita maafisa mipango miji wote wa halmashauri ili tukae nao, sababu hatutaki haya yaliyojitokeza yatokee tena, lazima miji yetu ipangwe vizuri,” amesema Waziri Ummy.

Tarehe 13 Septemba 2021, Rais Samia aliwaagiza wakuu wa mikoa nchini kuwapanga upya wamachinga katika maeneo rasmi.

Katika utekelezwaji wa agizo hilo, kuliibuka mvutano katika baadhi ya mikoa, hasa Dar es Salaam, ambapo wamachinga wa Soko la Kariakoo, waligoma kuondoka na kupelekea uongozi wa mkoa huo kutumia nguvu.

Kitendo hicho kiliwaibua baadhi ya wamachinga, na kuiomba Serikali itafute namna bora ya kuwapanga katika maeneo waliyokuwepo badala ya kuwaondoa na kuwapeleka katika maeneo rasmi, wakidai hawatafanya biashara kwa kuwa hakuna mzunguko mkubwa wa watu.

1 Comment

  • Asante ndugu ummy kauli imekubari hatuwezi kuishi kiolelaolela ni tanzania hapa duniania ndio iliolusu wamachinga wafanyebi ashara bira mpangilio hata sehem isiostahi waliweka bishara na wakapewa mamlaka makubwa and mamlaka sasa tunaldi tulipo toka tunaitaji dsm safi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

Habari Mchanganyiko

NMB yafuturisha Dar, Majaliwa azitaka Serikali za Mitaa, Taasisi zijifunze kwao

Spread the loveBENKI ya NMB imewafuturisha wateja wake walio kwenye Mfungo wa...

error: Content is protected !!