March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yafuta minada ya korosho

Spread the love

SERIKALI imefuta minada ya korosho hadi itakapotoa utaratibu mpya ifikapo tarehe 30 Oktoba 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hatua hiyo ya serikali imekuja baada ya minada mitatu katika msimu wa korosho wa mwaka 2018/2019 kukwama kutokana na wakulima wa zao hilo kugoma kuuza kufuatia kutoridhishwa na bei zilizofikiwa na kampuni zilizojitokeza katika minada hiyo.

Agizo la kufutwa kwa minada hiyo limetolewa leo tarehe 26 Oktoba 2018 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na viongozi wa mikoa inayolima korosho, katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Mnada wa korosho katika msimu wa 2018/19 ulizinduliwa rasmi Tarehe 22 Oktoba mwaka huu, huku tatizo la bei likiwa kikwako kikubwa kwa wakulima kuuza korosho. Katika mnada huo, bei ya juu ilikua Tsh 2717 na chini ikiwa Tsh 1711.

Kwenye mnada wa pili ulioendeshwa na Chama cha wakulima wa Mtwara na Masasi na Nanyumu (MAMCU) uliofanyika Wilayani Nanyumbu tarehe 23 Oktoba 2018, Wakulima waligoma kuuza Korosho zao kutokana na bei ya juu kuporomoka hadi Tsh 2520 kwa kilo na ya chini Tsh 2000, ikilinganishwa na bei ya mnada wa kwanza ambayo ilikua Tsh.1711 hadi Tsh.2717.

Baada ya Minada miwili ya mwanzo kugonga mwamba kufuatia wakulima Kugoma kuuza korosho zao kwa kutoridhishwa na Bei ya Tsh. 2717(mnada wa kwanza) na 2520(wa pili), mnada wa tatu uliofanyika Oktoba 24 2018, ulioendeshwa na Chama Cha Wakulima wa Korosho Wilaya za Ruangwa Nachingwe na Liwale(RUNALI) pia ulikwama.

Mnada huo wa tatu ulikwama baada ya bei ya korosho kutoridhisha wakulima, ambapo bei ya juu ilikuwa Tsh. 2657 na ya chini ikiwa Tsh. 2200.

error: Content is protected !!