Spread the love

 

SERIKALI imetoa ahueni kwa vyombo vya habari vya mtandaoni kwa kupunguza malipo ya ada ya leseni ya mwaka na kuwaondolea ada watoa maudhui ya burudani. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumzia mafanikio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye leo tarehe 14 Machi 2021 jijini Dar es Salaam amesema kuwa watoa maudhui ya burudani hawatatozwa ada.

Waziri Nape amesema Serikali imepitia na kurekebisha kanuni ya leseni ya maudhui ya burudani kwa ajili ya kukuza vipaji.

Ametoa mfano kwa wasanii wanaoweka maudhui ya nyimbo zao mitandaoni hawatalipia ada.

Akifafanau zaidi amesema watoa maudhui ya michezo na mapishi hawatalipa ada hiyo.

Nape ametanabaisha kuwa watoa maudhui ya habari na matukio ya sasa wamepunguziwa malipo ya ada kutoka Sh milioni moja kufika hadi Sh 500,000 na kwamba fomu ya maombi italipwa kwa Sh 50,000 badala ya Sh 100,000.

“Mmepiga kelele muda mrefu, kelele zenu Rais Samia amezisikia” amesema Waziri Nape.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *