Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yafunguka madai ya wanyamapori kutoroshwa kwa ndege
Habari za Siasa

Serikali yafunguka madai ya wanyamapori kutoroshwa kwa ndege

Serengeti
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imesema hakuna ndege zinazoingia katika hifadhi za taifa kwa ajili ya kutorosha wanyamapori, bali ndege zinazoingia hifadhini humo hutumiwa na watalii kwa ajili ya kuharakisha usafiri. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza katika mkutano uliofanyika mtandaoni leo Jumamosi, tarehe 14 Januari 2023, Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Pindi Chana, amesema viwanja vya ndege vilivyo katika hifadhi za wanyamapori vinalindwa kwa mujibu wa sheria.

“Hakuna mnyama aliyechukuliwa, tuko imara na salama wanyama wetu wanalindwa kisheria truliyojiwekea wenyewe. Naomba Watanzania watulie na taarifa kwamba kuna ndege imekuja imechukuwa wanyama, hakuna mnyama aliyechukuliwa, usafiri huu unaleta watalii kuja kutalii ndiyo maana tumeweka viwanja vya ndege,” amesema Balozi Pindi.

Balozi Pindi amesema, Serikali inalinda wanyamapori kwa mujibu wa sheria za nchi na mikataba ya kimataifa ambapo kwa sasa imeanza kufunga vifaa maalum vya kufuatilia mienendo yao wawapo hifadhini.

“Wanyama wetu wako salama na baadhi ya maeneo tumeanza kufunga vifaa tuna-watrack wanyama ikiwa pamoja na Tembo, tumetoka kwenye sensa ya wanyama Tanzania ni eneo ambalo lina nyati wengi ndani ya Afrika na ukiwa na nyati wengi ni uhakika wa chakula cha Simba ndiyo maana tuko juu, wizara tukasema tuwe na Jeshi la Uhifadjhi kulinda wanyama,” amesema Balozi Pindi.

Kauli hiyo ya Balozi Pindi Chana imekuja bnaada ya kuibuka taarifa katika mitandao ya kijamii, iliyodai kwamba kuna ndege imeingia kuchukua wanyama kwa ajili ya kuwapeleka nje.

1 Comment

  • Hakuna viwanja vya ndege kwenye hifadhi za Ulaya, Asia wala Amerika. Kwa nini Afrika tunababaishwa kama shamba la bibi? Watumie magari kwa sababu wanaenda kuangalia asilia siyo miji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!