Sunday , 25 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yafunga magazeti 3 kwa mwezi mmoja
Habari Mchanganyiko

Serikali yafunga magazeti 3 kwa mwezi mmoja

Toleo gazeti la Tanzania Daima lililokuwa na habari iliyosababishwa kufungiwa
Spread the love

UHURU wa vyombo vya habari hapa nchini umezidi kuingia matatani baada ya leo serikali kulifungia gazeti la kila siku la Tanzania Daima kwa siku tisini (90), anaandika Faki Sosi.

Katika kipindi cha takribani mwezi mmoja na siku nne serikali imefunga magazeti matatu yakiwamo ya MwanaHALISI, Raia Mwema na leo Tanzania Daima.

Kati ya Septemba 19 na Oktoba 24 mwaka huu serikali imeyafungia magazeti hayo.

MwanaHALISI lilifungwa kwa kuandika habari iliyokuwa na kichwa cha habari, ”Tumuombee Magufuli au Lissu, Raia

Mwema liliandika habari iliyosomeka Magufuli urais utamshinda na Tanzania Daima juzi liliandika kwamba asilimia 67 ya Watanzania wanatumia dawa za kurefusha maisha za ARVs.

Katika habari hiyo ya Tanzania ilionekana kuichukiza serikali na kusababisha Rais John Magufuli kuzungumzia suala hilo alipokuwa akiwatunuku vyeti wajumbe wa kamati za madini Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais alisema habari hiyo ni mbaya kwa taifa kwa sababu inaweza kusababisha wawekezaji wasije kuwekeza nchini kutokana na kuhofia wapi wanaweza kupata wafanyakazi kwa sababu itaonekana Watanzania wengi wanaumwa.

Taarifa ya kuchukuliwa hatua kwa gazeti hilo imechapishwa na Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Dk Hassan Abbasi.

Mmoja wa wahariri wa gazeti hilo, Saleh Mohammed amethibitisha kufungiwa gazeti hilo kwa muda wa siku 90.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari Mchanganyiko

“Jamii ielimishwe faida za uhifadhi”

Spread the loveWIZARA ya Maliasili na Utalii imesema ili kukabiliana na migongano...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza Nathwani alivyomshambulia jirani yake

Spread the loveSHAHIDI ambaye ni fundi Seremala, Dominic Mpakani (43) ameileza mahakama...

Habari Mchanganyiko

DCEA, TAKUKURU waunganisha nguvu kupamba na dawa za kulevya, rushwa

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!