October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yafumua mfumo wa Vyuo vya Afya

Dk. Zainab Chaula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya

Spread the love

WIZARA ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imefumua mfumo wa uongozi wa vyuo vya afya vidogo, ili kuboresha utoaji wa taaluma nchini. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).

Hatua hiyo imechukuliwa na Dk. Zainab Chaula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, katika mkutano wa wakuu wa vyuo vya afya 37, uliofanyika jijini Dodoma.

Dk. Chaula ameunganisha vyuo hivyo, na kupelekea idadi ya vyuo hivyo kupungua, kutoka vyuo 37 hadi kufikia tisa.

 “Wizara imeona ili kuboresha utoaji taaluma katika vyuo vyake,  ni vyema kubadilisha mfumo uliopo wa kuendesha vyuo vidogo vidogo. Na kutengeneza mazingira ya kuwa na vyuo vikubwa vichache, vyenye mfumo mzuri wa kiuongozi,  ili kuzalisha Wataalamu sahihi”, amesema Dk. Chaula.

Dk. Chaula amesema wizara ya afya imechukua hatua ya kufumua uongozi wa vyuo hivyo, baada ya kupokea changamoto mbalimbali, ikiwemo changamoto za uendeshaji wa mafunzo vyuoni uliotokana na uhaba wa watumishi na vifaa vya kufundishia.

error: Content is protected !!