Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Serikali yafanya msako uuzaji mbolea
Habari Mchanganyiko

Serikali yafanya msako uuzaji mbolea

Mifuko ya mbolea
Spread the love

MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea nchini (TFRA) imewataka wafanyabiashara wakubwa na wa kati kuzingatia bei elekezi ya uuzaji wa mbolea na uhifadhi wake kama taratibu zinavyoelekeza ili wakulima waweze kupata mavuno mengi na kukuza pato la taifa, anaandika Christina Haule.

Agousti 18, mwaka huu, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba alitangaza bei elekezi ya uuzaji wa mbolea nchini, baada ya kodi mbalimbali za uingizaji kuondolewa.

Amesema mfanyabiashara yeyote atakayebainika kuuza mbolea kinyume na bei elekezi iliyotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, atachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani mara moja.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkaguzi wa Mbolea wa mamlaka hiyo, Raymond Konga, wakati wa oparesheni ya kuwabaini wafanyabiashara ambao hawafuati bei elekezi ya uuzaji wa mbolea kwa wakulima.

Konga amesema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kukagua na kuangalia kama wafanyabiashara wa mbolea wanafuata bei elekezi katika kuelekea msimu wa kilimo mwishoni mwezi huu.

“Sisi hapa leo tunakagua kama bei elekezi ya mbolea ya kupandia na kukuzia mazao inafuatwa na kama mlivyojionea wenyewe, baadhi ya wafanyabiashara ikiwemo kampuni ya Matuyuni Agrochemical wao tumebaini wanahifadhi vibaya mbolea yao,”.

“Baada ya hali hiyo tumeamua kuchukua hatua ya kufunga ghala la kuhifadhia mbolea, kwa sababu mmiliki huyu (Matuyani Laizer) anahifadhi chini ya sakafu kinyume na taratibu zinavyoelekeza uhifadhi wa mbolea lazima iwekwe juu ya mbao,” amesema Konga.

Konga amesema ukaguzi huo ambao umeanzia mkoa wa Shinyanga na kuendeshwa katika wilaya zake zote, amesema utakuwa endelevu na utafika katika mikoa ya kanda ya ziwa na nchi nzima  kwa ujumla.

Bei elekezi iliyotolewa na Serikali kwa uuzaji wa mbolea aina ya DAP kwa jiji la Mwanza ni Sh. 55, 438 na mbolea aina ya UREA ni Sh. 42, 859.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Ditopile aungana na Wana-Kongwa kwa Iftar, wamuombea dua Rais Samia

Spread the loveKATIKA muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mbunge wa Viti...

Habari Mchanganyiko

PSSSF yawekeza kwenye viwanda 4, kuzalisha ajira 3,000

Spread the loveKATIKA kuisaidia Serikali kupunguza tatizo la uhaba wa ajira nchini,...

Habari Mchanganyiko

Luhemeja ahimiza utunzaji rasilimali maji kwa faida ya vizazi vijavyo

Spread the love  NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja...

Habari Mchanganyiko

NSSF yawapa darasa wahariri uwekezaji wa nyumba, yapewa cheti

Spread the loveMFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetoa wito...

error: Content is protected !!