Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yachukua hatua kukabili virusi vya Corona
Habari Mchanganyiko

Serikali yachukua hatua kukabili virusi vya Corona

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Spread the love

SERIKALI imejipanga kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona, kwa kuanza ukaguzi wa watu wanaoingia nchini, pamoja na kuanzisha maeneo ya kutibu wagonjwa endapo vitaikumba Tanzania. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo amesema Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati akizungumza na wanahabari leo tarehe 29 Januari 2020.

Waziri Ummy amesema serikali imejipanga kufanya uchunguzi kwa abiria wanaoingia nchini kupitia Viwanja vya Ndege vya Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), Kiwanja cha Ndege Mwanza na Kilimanjaro.

“Wizara imeendele akuchukua na kupima sampuli kutoka maeneo ya ufuatiliaji na yeyote atakayehisiwa sampuli zitapelekwa katika maeneo rasmi ya kupimiwa, “ amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy ametaja Hospitali zitakazotibu ugonjwa huo ni, Hospitali ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro, Kituo cha Udhibiti wa Magonjw aya Kuambukiza Mwanza na Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Aidha, Waziri Ummy amewaagiza Waganga wakuu kote nchini kuhakikisha wanajipanga vyema kukabiliana na changamoto hiyo.

“Mganga mkuu amelekeeza waganga wa mikoa kuchuku tahadhari kwa kupima maambukizi,” amesema Waziri Ummy.

Mlipuko wa Virusi vya Corona ulianza nchini China ambapo uliuwa watu 106na kuambukiza watu zaidi ya 4,000.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!