Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yachambua miradi ya Magufuli
Habari za Siasa

Serikali yachambua miradi ya Magufuli

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imeeleza hatua ilizofikia katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati, iliyoachwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli, aliyefariki dunia akiwa madarakani tarehe 17 Machi 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Magufuli aliyeiongoza Tanzania kwa muda wa miaka mitano na miezi mitano mfululizo (Novemba 2015 hadi Machi 2021), alifariki dunia kwa ugonjwa wa moyo, katika Hospitali ya Mzena mkoani Dar es salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu.

Mwili wake ulizikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita tarehe 26 Machi 2021.

Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma, leo Jumamosi tarehe 5 Juni 2021, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema utekelezwaji wa miradi hiyo unakwenda vizuri.

“Miradi inakwenda vizuri na utekelezaji wake unaendelea. Pamoja na kwamba nchi yetu imepita kwenye mabadiliko ya uongozi wa wakuu wa nchi, lakini miradi inatekelezwa kama tulivyojipangia na hali ya utekelezaji ni nzuri,” amesema Msigwa.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa

Kufuatia kifo cha Magufuli, aliyekuwa Makamu wake wa Rais, Samia Suluhu Hassan, tarehe 19 Machi mwaka huu, aliapishwa kuchukua mikoba yake na kufanikiwa kuwa Rais wa Awamu ya Sita wa Tanzania.

Msigwa amesema, Serikali ya Rais Samia, kuanzia Machi hadi Juni 2021, imetoa zaidi ya Sh. 2.6 trilioni, kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa miradi hiyo.

Akiichambua miradi hiyo, Msigwa amesema ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere (JNHPP-MW2115), katika Mto Rufiji, ulioanza Juni 2017, umefikia asilimia 52.

“Bwawa la Nyerere katika Mto Rufiji unaendelea kutekelezwa, Serikali imetoa Sh. 542 bilioni. Kazi za ujenzi zinaendelea wamefikia asilimia 52,” amesema Msigwa.

Msigwa amesema, mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro umefikia asilimia 91, wakati ujenzi wa kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma, umefikia asilimia 61.

“Serikali imeshatoa Sh 372 bilioni , kwa ajili ya kazi ya ujenzi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro yenye urefu wa kilomita 300, uliofikia asilimia 91,” amesema Msigwa.

Bwawa la Umeme Rufiji

Msigwa amesema, kwa sasa Serikali inaanza ujenzi wa kipande cha tano cha SGR, kuanzia Mwanza hadi Isaka mkoani Tabora. Na kwamba, vipande vilivyosalia vitatekelezwa baadae.

Msigwa amesema, mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigongo Busisi mkoani Mwanza, unaogharimu Sh. 712 bilioni, umefikia asilimia 27.

Hali kadhalika, amesema Serikali imeshatoa Sh. 659 bilioni, kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege, barabara na madarajka katika maeneo mbalimbali. Pia imetoa Sh. 17 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!