October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yabanwa bungeni wanafunzi walioacha shule

David Silinde, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Spread the love

 

SERIKALI imeagiza maofisa elimu katika halmashauri zote nchini kusimamia na kutekeleza ipasavyo muongozo wa kuwarejesha shuleni wanafunzi walioacha au kukatishwa masomo kwa sababu mbalimbali ili kutekeleza kwa asilimia 100 agizo hilo la Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Apaikunda Mosha TUDARCo … (endelea).

Silinde amesema mkakati wa serikali ni kuhakikisaha muongozo huu unasimamiwa na jukumu la Ofisi ya Tamisemi itahakikisha na kufuatilia utekelezaji wa muongozi huu na tathmini tutarudi na kuagiza maofisa elimu kuhakikisha kwamba agizo la rais Samia linatekelezwa wa muongozo huu kwa asilimia mia moja.

Pia Serikali kwa kushirikiana na bunge imepanga kuandaa sheria itakayolandana na agizo hilo ili kuwalinda watoto wanaoacha shule kwa sababu mbalimbali.

Hayo yameelezwa leo tarehe 14 Septemba, 2022 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, David Silinde wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu, Zaituni Seif Swai (CCM) aliyetaka kufahamu kauli ya Serikali juu ya sintofahamu ya utaratibu wa kuwapata wanafunzi wanaorudishwa masomoni.

Katika swali la nyongeza, Mbunge huyo alihoji mkakati wa Serikali kusimamia muongozo huo kwani utekelezaji wake ni mdogo katika katika halmashauri nyingi.

Pia alihoji, “Je, serikali haioni haja kutunga sheria kuhusu jambo hili ili kunusuru wanafunzi wetu?

Akijibu maswali hayo, Silinde amesema serikali kupitia wizara ya elimu, sayansi na teknolojia imetoa muongozo wa kuwarejesha wanafunzi waliokatisha masomo katika elimu ya msingi na sekondari kutokana na sababu mbalimbali ili waweze kukamilisha mzunguko wa elimu katika ngazi husika.

Amesema mkakati wa serikali ni kuhakikisha muongozo huo unasimamiwa na Tamisemi itahakikisha na kufuatilia utekelezaji wa muongozi huu na tutarudi na kuagiza maofisa elimu kuhakikisha kwamba agizo la Rais Samia linatekelezwa kwa asilimia mia moja.

Aidha, akizungumzia kuhusu kutungwa kwa sheria, Silinde amesema ni wazo jema,

“Tumelipokea na serikali kushirikiana na Bunge tutafanya mchakato kuhakikisha sheria hiyo inaletwa bungeni ili tuwalinde watoto ambao wameacha shule,” amesema.

error: Content is protected !!