Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yaazimia kuongeza uzalishaji kwa kusambaza mbegu bora
Habari Mchanganyiko

Serikali yaazimia kuongeza uzalishaji kwa kusambaza mbegu bora

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Wiebe De Boer
Spread the love

 

SERIKALI imesema katika kuboresha sekta ya kilimo ikiwemo kuongeza mnyororo wa thamani imeongeza bajeti yake mara mbili zaidi kutoka Sh bilioni 228 hadi Sh bilioni 751 mwaka 2022/23. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa mkoani Arusha na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Gerald Mweli,kwa niaba ya Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, katika mkutano wa wadau wa mbegu hapa nchini, ulioandaliwa na Kituo cha utafiti cha Kimataifa cha  World Vegetable Centre kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi nchini Tanzania.

Alisema miongoni mwa vipaumbele vyake ni pamoja na kuboresha uzalishaji na usambazaji wa mbegu ambapo imetenga Sh bilioni 300 kwa ajili ya skimu za umwagiliaji.

Naibu huyo alisema kuendelea kuimarisha tafiti kwa ajili ya upatikanaji wa mbegu bora, uwepo wa masoko utasaidia kupunguza vikwazo kwenye sekta hiyo na kuwa kikao hicho ni alama kwamba wadau na washirika wa maendeleo wako tayari kuendelea kushirikiana na serikali.

Kuhusu mbegu alisema kuwa itafanya uchunguzi na kuangalia mifumo yake na namna ya kushirikiana na wadau katika udhibiti wa mbegu bora hapa nchini.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli, akifunga mkutano huo

Alisema uwepo wa mbegu feki unaathiri kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara na wakulima wanapopata mbegu hizo zinawaathiri na kushindwa kupata mazao waliyoyategemea na kuwa mbegu bora zinatoa uhakika wa chakula na usalama wa nchi.

“Kupatikana kwa mbegu bora kunaandaa mazingira mazuri ya biashara hivyo usambazaji wa mbegu na uwepo wa mbegu feki katika masoko unaathiri wafanyabiashara, mbegu feki zinapomfikia mkulima zinatuathiri sana hawapati mazao tunayoyategemea”, alisema

“Jambo hili tunaenda kulifanyia kazi kwa kufanya uchunguzi na kuangalia mifumo yetu ya serikali ni jinsi gani inaweza kuahirikiana kudhibiti mbegu hizo na kama mna majawabu kwenye masuala hayo serikali ipo tayari kusikia na kuyafanyia kazi,”

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Wiebe De Boer,alisema madhumuni ya mkutano huo ni kujadili hali ya mbegu bora  nchini Tanzania na matumizi ya mbegu bora,kuangalia changamoto zinazokabili sekta hiyo na namna ya kuzitatua ili kuiboreshaji wa sekta hiyo ambayo ni muhimu katika kuongeza mavuno na usalama wa chakula.

Alisema faida za upatikanaji na matumizi ya mbegu bora,uboreshwaji wa mazingira ya biashara katika sekta hiyo utasaidia kukuza sekta hiyo na kuwa nchi hiyo iko tayari kutoa utaalamu wake juu ya masuala ya mbegu wakiamini kuwa mavuno mazuri huanza na mbegu bora.

Alisema anafurahi kuona wataalamu wengi wa masuala ya mbegu wakikutana kwa pamoja na kujadiliana juu ya namna ya kuboresha sekta hiyo.

Mkurugenzi wa taasisi inayojishughulisha na kilimo cha maua,mboga ,matunda,viungo na mazao yatokanayo na mizizi (TAHA), Dk. Jackline Mkindi, katika mkutano huo.

Alisema serikali ya nchi yake itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na sekta binafsi katika kukuza kilimo.

Naye Mkurugenzi wa Kanda wa Kituo hicho, Dk Gabriel Rugalema,alisema upatikanaji na matumizi bora ya mbegu ni muhimu kwa ukuaji wa nchi yoyote.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara wa Mbegu Tanzania(Tasta),Bob Shuma,alisema kazi yao kubwa ni kushirikiana na serikali kwa kuhakikisha nia za serikali na wawekezaji zinakamilika na wananchi wanapata mbegu bora.

Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa mbogamboga na matunda cha Kimataifa cha World vegetables Center, Dk. Gabriel Rugalema, akizungumza katika mkutano huo

Alisema kunapokuwa na chakula kingi katika nchi ni kwa sababu ya ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi ambazo kwa pamoja zinahakikisha mkulima anapata mahitaji yake.

“Pamoja na mambo mengine tumejadili na kuhakikisha ubora wa mbegu ambazo zinazalishwa hapa nchini zinapelekwa nje ya nchi pamoja na zile zinazouzwa hapa nchini,”alisema

“Ubora wa mbegu ni muhimu hivyo lazima tuweke mifumo mizuri,tumeangalia tumetoka wapi,tumefika wapi na tunaelekea wapi kuhakikisha yaliyofanyiwa kazi yatazidi kuwepo na utafiti unaongezeka,tumezungumzia juu ya wawekezaji wa ndani kwa mfano tuna makampuni za wazawa walioanzisha kampuni za mbegu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!