Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya Serikali yaanza kuikabili Dengue
Afya

Serikali yaanza kuikabili Dengue

Mbu wanaambukiza ugonjwa wa Dengue
Spread the love

SERIKALI imesema, imekusanya watalaamu kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuangamiza mbu, ikiwa ni hatua za awali za kupambana na ugonjwa wa Dengue. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 19 Juni 2019 na Ummy Mwalimu ambaye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto alipojibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (CCM).

Katika swali lake Zungu alitaka kujua, ni kwanini serikali isitoe dawa za chenga kwa viongozi wa mitaa ili waweze kumwaga katika maeneo yao kuua mbu na mazalia yake.

“Hawa mbu hivi sasa wanaingia majumbani, kwenye mabasi na hata katika masanduku sasa ni kwanini serikali ikatoa dawa za chenga na kuzigawa kwa viongozi wa mitaa ili waweze kumwaga kuua mbu na mazalia yake” amesema.

Ummy amesema, tayari dawa mbalimbali zinatumika katika kudhibiti ugonjwa huo kwa sasa.

Amesema, hakuna njia nyingine katika kudhibiti ugonjwa huo zaidi ya kuua mbu na mazalia yake.

“Tumesha wakusanya watalaamu wa kuangamiza mbu toka sehemu mbalimbali, kuangalia njia mbalimbali za kupambana na mbu lakini inaonekana mbu hawa ni sugu,” amesema.

Awali akijibu swali la msingi la Neema Mgaya, Viti Maalum (CCM), Naibu Waziri wa Wizara hiyo Faustine Ndugulile amesema, wametoa fursa kwa watumishi 400 ambao wapo katika vyuo mbalimbali kusomea huduma za kutoa dawa za usingizi.

Ndugulile anasema, miongoni mwa watumishi hao wanatoka Mkoa wa Njombe.

Ameeleza kuwa, mara watakapohitimu kozi hiyo Mkoa wa Njombe pia utanufaika kwa kuimarisha huduma huduma ya dawa za usingizi katika Hospitali mbalimbali zilizopo katika Mkoa wa Njombe.

Amesema, katika kipindi cha mwaka 2018/2019, Mkoa wa Njombe katika vyanzo vyake ulisomesha wauguzi watano kutoka Halmashauri ya Ludewa (2),Makete (1), Wangiing’ombe (1),na Njombe (1) kwa kozi ya mwaka mmoja .

Amesema, katika ngazi ya Hospitali ya Mkoa umepeleka madaktari wawili kusoma Shahada ua Uzamivu wa Dawa za Usingizi na ganzi, ili kuimarisha huduma za wagonjwa mahututi.

Katika swali lake Neema alitaka kujua, ni lini serikali itatatua changamoto ya madaktari wa dawa za usingizi katikaMkoa wa Njombe?.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

AfyaTangulizi

Wanasayansi wagundua teknolojia ya kunyofoa VVU kutoka kwenye seli

Spread the loveTIMU ya wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam cha nchini...

Afya

Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8

Spread the love  SERIKALI imetoa Sh 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi...

error: Content is protected !!