July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yaanika mkakati kubana matumizi “tutapimiana mafuta ya magari”

Gari aina ya Toyota Land cruiser V8

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imetangaza mkakati wa kubana matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, ili yaakisi ugumu wa maisha wanayopitia wananchi kufuatia athari za janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mkakati huo umetangazwa leo Jumanne na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.

Dk. Mwigulu ametaja hatua zitakazochukuliwa ndani ya muda mfupi katika suala hilo, ikiwemo Serikali kuanza kuwapimia mafuta ya magari watumishi wa umma ili kudhibiti matumizi hayo kila mwezi.

“Hatua za muda mfupi zitakazochukuliwa ni pamoja na kupunguza safari za ndani na nje, kukata fedha za ununuzi usio wa lazima, kupunguza ukubwa wa uwakilishi kwenye mikutano ya ndani na nje, tutapimiana mafuta ya magari ya Serikali kila mwezi kufuatana na shughuli za lazima. Utaratibu huu unatumika haa kwa wabunge na hawajahi kuacha kufanya ziara,” amesema Dk. Mwigulu.

Waziri huyo wa fedha amesema “nimemuelekeza mlipaji mkuu wa Serikali afanye uchambuzi wa wastani wa mahitaji ya mafuta kufuatana na aina ya majukumu, ulazima wa majukumu pamoja na ngazi katika utumishi.”

Akitangaza hatua za muda wa kati na mrefu, Dk. Mwigulu amesema Serikali inakusudia kubadili utaratibu uliokuwepo wa ugawaji magari ya watumishi wa umma, kwa kuanza kuwapokesha wale wenye hadhi ya kuwa na magari, ambayo watayahudumia ikiwemo katika matengenezo na ununuiz wa vipuri.

“Wawe na magari yao wenyewe, walipiue wafanye matengenezo wao wenyewe, wanunue vipuri na masuala ya mafuta yaangaliwe kwa utaratibu utakaoonekana unafaa. Wapate magari yao watasimamia vizuri matengezo na mafuta” amesema Dk. Mwigulu.

Waziri wa Fedha na Mpango wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba

Amesema, mikakati hiyo ikianza kutekelezwa, Serikali itaokoa zaidi ya bilioni 500 kila mwaka, ambazo zitapelekwa katika kutoa huduma za kijamii kwa wananchi.

“Kama utaratibu hup wa kuwakopesha watumishi wenye stahili za magari na gharama za matumizi na mambo mengine, gharama za matumizi ya Serikali zitashuka kutoka bilioni 550 kwa mwaka hadi bilioni 50.5,” amesema Dk. Mwigulu.

error: Content is protected !!