Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yaagiza magari ya wagonjwa 258
Habari za Siasa

Serikali yaagiza magari ya wagonjwa 258

Gari la wagonjwa
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema katika kuboresha huduma za afya nchini Serikali imeagiza magari ya wagonjwa 258 yakiwemo 233 ya kawaida na 25 ya kisasa. Anaripoti Mwandishi Wetu Dodoma … (endelea).

Ameyasema hayo leo Jumatano tarehe 6 Aprili 2022 jijini Dodoma, akizindua mfumo wa usafirishaji wa dharura wa wajawazito na watoto wachanga (M-Mama).

Mbali na magari ya wagonjwa Rais Samia amesema wameagiza pia magari 242 kwaajili ya uratibu na kusema kuwa anaamini yataongeza nguvu katika mfumo huo wa M-Mama.

Ameongeza kuwa kuwepo kwa mfumo wa anwani za makazi nako kutasaidia ufanisi wa M-Mama kwani iamrahisishia mjamzito kutoa taarifa vizuri za mahali alipo.

“Anwani za makazi itarahisisha simu inapopigwa kusema nipo mtaa fulani nyumba fulani,” amesema Rais Samia.

Amesema pia Serikali “tumemwaga fedha nyingi kwa Tarura ili kuboresha huduma za barabara zipitike kwa misimu yote Tanzania kote.

“Ni matumaini yetu mambo yote haya yatakwenda kuboresha huduma za afya.”

Mfumo wa M-Mama unakwenda kusambazwa katika mikoa 14 ya Tanzania bara ikitarajiwa kuhudumia wajawazito milioni moja na baadae itafikishwa hadi visiwa Zanzibar.

Mfumo huo umeanzishwa kwa majaribio mwaka 2013 katika wilaya za Sengerema na Shinyanga na imefikia zaidi ya wajawazito 12,000.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

error: Content is protected !!