Tuesday , 5 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Serikali ya Umoja wa Kitaifa yanukunia DRC
Kimataifa

Serikali ya Umoja wa Kitaifa yanukunia DRC

Felix Tshisekedi, Rais wa DR Congo
Spread the love
RAIS mteule wa DRC- Kongo, Felix Tshisekedi Tshilombo, mtoto wa mwanasiasa mkongwe  nchini Ettiene Tshisekedi, ameridhia uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa nchini mwake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Tshisekedi alitangazwa na Tume ya uchaguzi nchini DRC-Kongo, kuwa mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi wa 30 Desemba 2018.
Taarifa kutoka kwa watt waliokaribu na kiongozi huyo zinasema, hatua hiyo inafuatia ushindi wake kugubikwa na madai mazito ya udanganyifu kwenye uchaguzi na nguvu kubwa aliyonayo washindani wake wa kisiasa.
Katika uchaguzi huo, Martin Fayulu (61), anadai kuwa ndiye aliyekuwa mshindi halali wa kiti cha urais. Anamtuhumu Rais Joseph Kanabe Kabila, kusaidia kufanikisha wizi wa kura na udanganyifu katika uchaguzi huo.
Matokeo hayo yaliyomtangaza Tshisekedi kuwa mshindi wa kiti cha urais, yamepingwa hadharani na Baraza kuu la Maaskofu wa kanisa Katoliki (CENCO), nchini humo. Kanisa Katoli, ndilo lenye ushawishi mkubwa nchini DRC.

Katika taarifa take kwa vyombo via habari, Kanisa linasema, lilisambaza wachunguzi wake 40,000 Katina uchaguzi duo niching kote. Limepata matokeo, na kwamba “kilichotangazwa siyo matakwa halisi ya wananchi.”

Maelezo ya Kanisa Katoli yanaungwa mkono na mataifa kadhaa makubwa ulimwenguni, ikiwamo Marekani, Ufaransa na Ujerumani.

Tayari Fayulu ameiomba jamii ya kimataifa kutotambua Tshisekedi kama rais wa nchi hiyo. Ametaka pia kutoyatambua matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na ametoa wito kwa wafuasi wake, kufanya maandamano.

Fayulu anaamini kwamba kura zake ziliibwa, huku data ilioibwa ikionyesha kuwa alipata kura mara tatu ya kura alizopata Tshisekedi.

Muungano wa Afrika (AU), ulisema siku ya Ijumaa iliyopita kuwa kulikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya uhalali wa matokeo hayo na kutaka matokeo rasmi kucheleweshwa kutangazwa.

Mahakama ya kikatiba nchini DR Congo imeidhinisha ushindi wa Tshgisekedi, Jumamosi iliyopita. Mahakama ilisema kuwa Fayulu alishindwa kuthibitisha kuwa tume ya uchaguzi ilitangaza matokeo bandia.

Tume ya uchaguzi awali ilikuwa imetangaza kwamba Tshisekedi alikuwa amepata asilimia 38.5 ya kura hizo. Fayulu alipatia asilimia 34.7 na mgombea wa chama tawala, Emmanuel Shadary alipata asilimia 23.8.

Fayulu alijitosa kwenye kinyang’anyiro hicho kwa kuungwa mkono na viongozi wakuu wa vyama saba vya upinzani. Mazungumzo ya viongozi hao yalifanyika mjini Geneva nchini Uswiss.

Kiongozi huyo kutoka chama cha upinzani cha Ecidé, hakuwa miongoni mwa watua waliokuwa wanapewa nafasi ya kuchukuwa na fasi hiyo.

Fayulu, hakuwa maarufu katika siasa ndani na nje ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na wala hakuwa anafahamika miongoni mwa wanasiasa wakuu wa upinzani nchini humo.

Hata hivyo, alishiriki kikamilifu na alikuwa kiungo muhimu katika harakati za kuendesha maandamano makubwa yaliyoikumba DRC tangu mwaka 2015 na kuonekana mmoja kati ya watu wanaopinga rais Joseph Kabila kuwania muhula wa tatu wa uongozi.

Wagombea wa upinzani ambao walikuwa wameorodheshwa kuwania urais huko Geneva, ni pamoja na Felix Tshisekedi, Vital Kamerhe, Martin Fayulu na Freddy Matungulu. Mazungumzo ya wapinzani yalisimamiwa na Wakfu wa Kofi Annan, aliyewahi kuhudumu katika nafasi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN).

Inaarifiwa kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2011, Fayulu alimfanyia kampeni kiongozi wa upinzani marehemu Ettiene Tshisekedi.

Martin Fayulu, mbali ya kujihusisha na masuala ya kisiasa ni mfanya biashara maarufu nchini Congo. Miongoni mwa vitega uchumi vyake ni umiliki wa hoteli.

Alisomea nchini Marekani na Ufaransa. Aliwahi kufanya kazi katika makampuni makubwa ya simu nchini Marekani.

Aliwahi kukamtwa mara kadhaa katika maandamano ya upinzani nchini humo.

Fayulu aliungwa mkono katika harakati zake za kutafuta Ikulu na mbabe wa zamani wa kivita nchini humo, Jean-Pierre Bemba, ambaye alizuiwa kugombea nafasi hiyo na tume ya uchaguzi.

Bemba alikuwa miongoni mwa wagombea sita waliokuwa wamewasilisha majina yao kutaka kugombea nafasi hiyo.

Kiongozi huyo wa zamani wa waasi aliachiliwa huru baada ya mahakama kubatilisha hukumu dhidi yake ya kumpata na hatia ya uhalifu wa kivita mwezi Juni mwaka jana.

Tume ya uchaguzi ilidai kuwa Bemba amezuiwa kuwania urais kwa kuwa alipatikana na hatia ya kuwahonga mashahidi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).

Bemba, aliyerejea DR Congo mwanzoni mwa Agosti baada ya kukaa uhamishoni miaka 11 au gerezani, aliamua kumuunga mkono Fayulu kufuatia kushindwa rufaa yake ya kupinga kuenguliwa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Vilevile, Fayulu aliungwa mkono na Moise Katumbi, gavana wa zamani wa Katanga.

Kufuatia hali hiyo na kile kilichotokea kwenye uchaguzi wa 30 Desemba, taarifa zinasema, Rais  Tshisekedi, ameona njia pekee ya kuinusuru DRC-Kongo, ni kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Tshisekedi amekubali kumteuwa Fayulu kuwa waziri wa fedha; Bemba waziri wa mambo ya nje na Katumbi kuwa waziri mkuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Muandamanaji ajichoma moto akipinga vita Palestina, Israel

Spread the loveMUANDAMANAJI moja ambaye hajafahamika jina, yuko mahututi hospitalini akitetea uhai...

Kimataifa

Urusi kuongeza wanajeshi ikijihami dhidi ya NATO

Spread the loveSERIKALI ya Urusi iko katika mpango wa kuongeza wanajeshi wake,...

Kimataifa

Israel yarejesha mashambulizi Gaza ikilaumu Hamas kukiuka makubaliano

Spread the loveJESHI la Israel, limerejesha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, baada...

Kimataifa

Papa Francis kumfukuza Kardinali anayepinga mageuzi Kanisa Katoliki

Spread the loveKIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, anadaiwa kupanga kumfumkuza...

error: Content is protected !!