Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Bobi Wine aachiwa huru, akamatwa tena
KimataifaTangulizi

Bobi Wine aachiwa huru, akamatwa tena

Bobi Wine
Spread the love

SERIKALI ya Uganda imemuondolea mashtaka Mbunge wa Kyadondo, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, lakini alikamatwa tena muda mfupi baada ya kuachiwa huru. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Bob Wine leo Alhamisi tarehe 23 Agosti, 2018 alitarajiwa kurudishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu Kaskazini mwa Uganda.

Uamuzi huo unadhaniwa kushinikizwa na hatua ya jumuiya za kimataifa zilizoishinikiza serikali ya Uganda kumuachia huru Bob Wine.

Kabla ya Serikali ya Uganda kutangaza kumuondolea mashitaka Bob Wine, mawakili wake walijuzwa kuwa kesi ya mwanasiasa huyo machachari itasikilizwa katika kambi ya Kijeshi ya Makindye alikokuwa anazuiliwa Bob Wine.

Muda mfupi baada ya kuachiliwa huru, Wine alikamatwa tena na inaarifiwa kwamba anatarajiwa kushtakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu kujibu mashtaka ya uhaini pamoja na wabunge wengine waliokamatwa.

Mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki nchini kwa jina maarufu Bobi Wine leo aliwasilishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda.

Mawakili wake awali walijuzwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa mjini Kampala. Kumekuwa na shinikizo kubwa kimataifa la kutaka Bobi Wine aachiwe huru.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

error: Content is protected !!