Sunday , 3 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Serikali ya Tanzania yatoa utaratibu kumuaga Mkapa kesho
Habari Mchanganyiko

Serikali ya Tanzania yatoa utaratibu kumuaga Mkapa kesho

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Hayati Benjamin Mkapa
Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema, viongozi wakuu wa nchi kesho Jumanne ndio watapata fursa ya kuaga mwili wa Hayati Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Jumatano tarehe 27 Julai 2020 jioni mara baada ya kumaliza kuaga mwili wa Rais mstaafu Mkapa, katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuamzalia kuaga, Majaliwa alizungumza na waandishi wa habari akisema, Serikali ilitenga siku tatu kwa waombolezaji kufika kumuaga kiongozi huyo aliyeongoza Tanzania kwa miaka kumi mfululizo kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.

Mkapa alifikwa na mauti Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam kwa tatizo la mshituko wa moyo.

Majaliwa amesema, kati ya jana Jumapili na leo, ilikuwa ni fursa kwa watu mbalimbali kuaga mwili wa Mkapa kabla ya kesho kufanyika kwa shughuli ya kitaifa ya kumuaga itakayoongozwa na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli kuanzia saa 4 asubuhi.

“Kesho watakaopata fura ya kuaga mwili wa mpendwa wetu ni viongozi wa juu akiwemo Rais, Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar ambao wataungana na baadhi ya viongozi wa dini pamoja na wageni kutoka nchi jirani,” amesema Majaliwa

Majaliwa amewaomba Watanzania hususan wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo kesho ili kuhudhuria shughuli hiyo ya kitaifa.

Amesema, baada ya kumalizika, mwili wa Mkapa utasafirishwa kwenda kijijini kwake Lupaso, Masasi Mkoa wa Mtwara kwa maziko siku ya Jumatano tarehe 29 Julai 2020.

Majaliwa amesema, maziko hayo yatatanguliwa na wakazi wa maeneo hayo kuaga mwili huo kuanzia asubuhi hadi saa 7 mchana kasha taratibu za kuuhifadhi mwili huo katika makazi ya milele itaanza.

Awali, kabla ya Majaliwa kufika uwanjani hapo, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dk. Hassan Abbas alitoa utaratibu utakavyokuwa kesho Jumanne kwa waombolezaji kufika uwanjani hapo.

Dk. Abbas alisema utaratibu umeandaliwa usafiri utakaoanzia viwanja vya Kalimjee kwenda uwanja wa Uhuru utakaowabeba mawaziri, makatibu wakuu, mabalozi, wakuu wa mikoa na wilaya.

Wengine ni wakurugenzi, viongozi wa vyama vya siasa na wageni wengine waliopewa.

Dk. Abbas amesema, magari binafsi hayataruhusiwa na magari yatakuwa tayari kuanzia saa 12 asubuhi na gari la mwisho litaondoka katika viwanja hapo saa 1:30 asubuhi.

Msemaji huyo wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema, kabla ya mwili wa Mkapa kupelekwa uwanjani hapo, utaanza Kanisa Katoliki la Imaculata, Upanga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the loveMVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara...

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Habari Mchanganyiko

TARURA kujenga madaraja 189 kwa teknolojia ya mawe

Spread the loveWakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imejipanga kujenga...

AfyaHabari Mchanganyiko

Majaliwa aipongeza GGML mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveWaziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining...

error: Content is protected !!