May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali ya Tanzania yaonya wafanyabiashara ukwepaji kodi

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imetangaza kuanza kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara wanaowaongoza wananchi kukwepa kulipa kodi. Anariooti Noela Shila, TUDARCo … (endelea).

Onyo hilo limetolewa leo Ijumaa, tarehe 20 Agosti 2021 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Dk. Mwigulu amesema, hivi karibuni imeibuka tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kuwapunguzia bei wananchi wanaokubali kununua bidhaa zao bila kuchukua risiti, ili kujitengenezea mazingira ya kutokatwa kodi.

“Wafanyabiashara waache kuwaongoza Watanzania kukwepa kodi, ili eneo ukifika dukani mtu anakuuliza unataka kulipia hii bidhaa, anakwambia bei yenye risiti ni laki tano, isiyo na risiti laki tatu.”

“Hiki ni kinyume cha sheria, tukatae hawa wanaofundisha wananchi kukwepa kodi na wakiendelea tutawafikisha kwenye mikono ya sheria,” amesema Dk. Mwigulu.

Waziri huyo amewaomba wananchi wasijiingize katika mchezo huo kwa kuwa ni kinyume cha sheria, lakini pia kinaikosesha Serikali fedha za kuwahudumia.

“Penye manunuzi dai upewe risiti na wewe unayetaka kuweka punguzo kukwepa kodi ni uvunjifu wa sheria na sheria tumeweka kodi lazima ilipwe,” amesema Dk. Mwigulu na kuongeza:

“Unataka kuhamasisha asichukue risiti, ukiona hivyo anakufundisha kuvunja sheria kwa kukwepa kodi, usipochukua risiti wakati mwingine anachukua ile hela. Hivyo ile hela ya kuleta madawati na dawa anachukua yeye. Tukiwabani tutawachukulia hatua kali.”

error: Content is protected !!