Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari Serikali ya Tanzania yailipa MSD bilioni 39 kati ya 269
Habari

Serikali ya Tanzania yailipa MSD bilioni 39 kati ya 269

Spread the love

 

WIKI chache baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuitaka Serikali ya Tanzania ilipe deni la Bohari ya Dawa (MSD) kiasi cha Sh bilioni 269, Serikali tayari imelipa kiasi cha Sh.39 bilioni kwa wazabuni mbalimbali waliosambaza dawa za binadamu nchini. Anaripoti Mwandishi wetu (endelea…)

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa
leo Jumapili, tarehe 12 Septemba 2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Amesema mbali na fedha hizo, Serikali imetenga kiasi cha Sh.223 bilioni kuagiza dawa mbalimbali za binadamu nje ya nchi.

“Mpango wa kulipa madeni unaendelea. Tayari tumetoa Sh.200 bilioni kulipa madeni mbalimbali ikiwamo ya watumishi wa umma.”

“Serikali inaendelea kulipa taratibu kadiri uhakiki unavyofanyika kwa sababu dhamira yake ni kuhakikisha madeni nhaya yanalipwa,”amesema

Tarehe 20 Agosti 2021, Mwenyekiti wa Kamati ya PAC Naghenjwa Kaboyoka alisema madeni hayo ya MSD yanazorotesha shirika hilo.

“Serikali msipoilipa mnaifanya MSD ishindwe kufanya kazi kwa ufanisi, mwanzo nadhani waliacha kuwapa fedha kwa sababu kulikuwa na udanganyifu mkubwa lakini katika bajeti ya mwaka huu wamesema watyaanza kupunguza deni, tumesisitiza serikali ilipe madeni haya ili shirika lifanye kazi vizuri na kwa ufanisi,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!