SERIKALI ya Tanzania inampango wa kujenga shule 26 za wasichana na shule 1,000 za sekondari kwenye kata zisizo na shule hizo. Anaripoti Patricia Kighono, TUDARCo…(endelea).
Pia, itafanya upanuzi wa shule za sekondari 100 kuweza kupokea wanafunzi zaidi wa kidato cha tano na sita.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Tamisemi, David Silinde leo Alhamisi, tarehe 9 Septemba 2021, wakati akijibu swali la Mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Miraji Mataturu.
Mtaturi ameulia ni lini serikali itajenga shule ya sekondari ya kidato cha tano na cha sita Mungaa ambayo ni ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa kipindi cha kampeni mwaka 2020 alipopita jimbo la singida mashariki.
Akijibu swali hilo, Silinde amesema serikali inampango wa kujenga shule 26 za wasichana, moja katika kila mkoa na ujenzi wa shule 1000 za sakondari kwenye kata zisizo na shule za sekondari ili kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na vikwazo hususani watoto wa kike kutembea umbali mrefu.
Silinde amesema, serikali itafanya upanuzi wa shule za sekondari 100 kuweza kupokea wanafunzi zaidi wa kidato cha tano.
Pia amesema serikali imetenga kiasi cha Sh.220 bilioni kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa shule za sekondari ambao utafanyika kwa awamu. Awamu ya kwanza itaanza mwaka wa fedha 2021/2022. Kabla ya ujenzi kuanza serikali itafanya tathmini ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi huo ikiwemo shule ya sekondari Mungaa.
Naomba kuuliza.
Kwanini visijengwe viwanda, halafu mapato yajenge shule?